Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

MTAPOKEA MARA MIA ZAIDI



“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Jumanne, Mei, 30, 2023 
Juma la 8 la Mwaka wa Kanisa

YbS. 35 : 1-12; 
Zab 50: 5-8, 14, 23; 
Mk 10: 28-31


MTAPOKEA MARA MIA ZAIDI!


Injili inaongelea kuhusu wafuasi baada ya yule kijana tajiri kuongea na Yesu kuhusu kuurithi ufalme wa milele. Yesu alimualika aache mali yake yote amfuate. Lakini yule kijana aliondoka mbele ya Yesu kwa huzuni na moyo mzito. Wakiwa wanafikiri kuhusu wao wenyewe Mitume wanamuuliza Yesu swali kuhusu hatima yao ya baadae. Yesu anajibu kwakusema, “Amin, nawaambieni, Hakuna mtu aliyeacha nyumba, au ndugu waume, au ndugu wake, au mama, au baba, au watoto, au mashamba, kwa ajili yangu, na kwa ajili ya Injili, ila atapewa mara mia sasa wakati huu, nyumba, na ndugu waume, na ndugu wake, na mama, na watoto na mashamba, pamoja na udhia; na katika ulimwengu ujao uzima wa milele. Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho; na wa mwisho watakuwa wa kwanza.” 

Kwakuacha dunia ambayo kila mtu anapigania kupata sehemu ya ardhi, wengine wanapata sehemu kubwa hata hawajui wafanyie nini, wengine wanasehemu ndogo kiasi ambacho wanaji banabana, wengine hawana kabisa. Mkristo wa kweli mwenye roho ya Injili, anakuwa kwenye jumuiya ambayo kila mmoja anapaswa kujali wengine, na pale ambapo kila mmoja anaangalia hitaji la mwingine katika kushirikishana matunda aliyojaliwa na Mungu kama jumuiya. Hii ndio maana ya kuacha nyumba au familia na kuacha mali binafsi nakuingia katika familia mpya ambayo ina mama wengi zaidi, kaka wengi, dada wengi, ambapo hapo familia binafsi inakuwa imechukuliwa na familia ya watu kutoka jamaa mbali mbali, mkishirikishana upendo, matendo ya huruma kutoka familia hii kwenda familia hii.

Huu ndiyo ukweli, ambao kwa bahati mbaya, haujajulikana sana kwa wakristo wengi, wanaoishi maisha yao, kwakujitenga nakujali maisha yao binafsi zaidi wakidhani kwamba wakipata kitu kutoka kwa mtu mwingine bila ya wao kukifanyia kazi wanadhani wamedhalilishwa na hawatakifurahia.

Sala: Ee Bwana, tufundishe tusiwe wabinafsi katika kuwajali watu wako katika familia hii inayoitwa ulimwengu. Amina


Copyright ©2013-2023 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com

No comments:

Post a Comment