Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

FURAHI KATIKA BWANA!


“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya Pasaka
Alhamisi, Mei 9, 2024.
Juma la 6 la Pasaka

Mdo 18: 1-8; 
Zab 98: 1-4; 
Yn 16: 16-20

FURAHI KATIKA BWANA!

Bwana wetu katika Injili, anawaambia Wanafunzi wake kwamba bado kitambo kidogo watamwona na bado kitambo kidogo hawatamwona. Aliwaandaa kwa kifo na ufufuko wake. Anawaambia watalia na kuhuzunika wakati ulimwengu utakuwa ukifurahi, bali huzuni yao itabadilishwa na kuwa furaha. Kwahiyo wakati walivyokuwa wanamuona Bwana baada ya ufufuko ilikuwa nikukamilisha unabii juu yake. Kwa upande wa Ulimwengu itakuwa kinyume, furaha ya ulimwengu itageuka kuwa huzuni.

Yesu anawaambia wanafunzi wake kwamba huzuni na furaha itakuwa sehemu ya maisha yao ya kila siku. Ni kitendo cha upendo kwa upande wake, kuwa mbele ya wanafunzi wake kuhusu magumu watakayo kutana nayo mbele. Habari njema ni kwamba Yesu anasema usemi huu ukifuatana na usemi wa matumaini kwamba “huzuni yao itageuka kuwa furaha”. Ni wazi pia katika maisha yetu. Yesu hatupi ahadi kwamba maisha yetu yatakuwa ya furaha tuu bila magumu na huzuni. Hatuambii kwamba kumfuata yeye, kila kitu kitakuwa shwari na rahisi. Kama tutafuata njia zake tuwe tayari kuona magumu na uchungu ambayo ndio njia itakayo geuka na kuwa neema na furaha kwa wengi. Kama tutaweze kukabili magumu ya maisha kwa imani na matumaini, hakuna kitakacho tuweka chini na kila kitu kitaweza kutumika kwa utukufu wa Mungu na yataishia katika furaha kubwa.

Kilicho cha muhimu kwetu nikubaki tukiwa tunamwelekea Bwana kwasababu ni kutoka kwake na ni kutoka kwake upendo wote watoka, na ni kutoka kwake furaha yote yatoka. Furaha inayotokana na ulimwengu ni fupi na ya muda tu, tena inayopita. Hakuna kitu kinacho baki milele kinacho tokana na ulimwengu. Furaha inapatikana kwa Yesu pekee. Usihuzunishwe wala kukatishwa tamaa wakati maisha yanakuendea vibaya. Usipoteze matumaini wakati magumu yanapo tokea katika maisha yako. Kabidhi kila kitu kwa Bwana wetu na muache avigeuze viweze kuwa na furaha ile aliyoahidi mwishoni.

Sala: Bwana, ninakabidhi mateso yangu yote ya maisha yangu, mikonini mwako. Huzuni, magumu, mateso na kuchanganyikiwa nina jikabidhi mikononi mwako. Nina amini kwamba wewe ni mwenye nguvu na unatamani kubadili vyote katika utukufu wako. Nipe matumaini wakati wa kupoteza matumaini na kukutegemea wakati maisha yakiwa magumu. Yesu, nakuamini wewe. Amina

Copyright ©2013-2024 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com

No comments:

Post a Comment