“MBEGU ZA UZIMA”
Tafakari ya Kwaresima
Machi 3, 2024
------------------------------------------------
DOMINIKA YA 3 YA KWARESIMA
Somo la 1: Kut 20:1-17 Tunasikia kuhusu Amri amabazo Mungu anampa Musa katika mlima Sinai. Ni ramani ya watu katika maisha yao ambayo ina uhusiano wa pekee na Mungu.
Wimbo wa katikati: Zab 19:8-11 “Sheria ya Bwana nikamilifu, huburudisha moyo”.
Somo la 2: 1 Kor 1:22-25 Mt. Paulo anatoa kiini cha mahubiri yake kwamba ni Kristo msulubiwa. Kwa wengine swala la Yesu msulubiwa halina maana kabisa. Lakini kwa wote walionauwezo ni ishara ya hekima ya Mungu.
Injili: Yn 2: 13-25 Yohane anatoa hali ya jinsi Yesu alivyo safisha hekalu na jinsi Wayahudi walivyo lichukulia”.
------------------------------------------------
KUABUDU KWA ROHO YA KWELI
Katika somo la kwanza: anaongelea kuhusu amri zake kana kwamba mmoja atamzaa mtoto. Kwa maneno yake anawazaa watoto wapya, taifa jipya, na njia mpya ya maisha, na kuandaa maisha mapya ya kutoka jangwani na kulilinda kundi. Amri kumi za Mungu zinakuwa ni kiini cha uhusiano wa Wayahudi na Mungu na kati yao wenyewe. Kwa Wakristo hali ya kuwatoa watu utumwani na kuwaleta katika nchi ya ahadi inafanyika kwa njia ya ubatizo na kwa njia ya kifo cha Kristo. Tunatimiza sasa amri za Mungu kama vile Yesu alivyofanya katika maisha yetu kwa kuwa kioo cha jamii husika kwa kuwatoa watu utumwani na kuwafanya kuwa huru. Amri zinawakilisha utakatifu wa Mungu kati ya watu wa Mungu.
Katika wimbo wa katikati unatupa muhtasati mzima wa masomo”Bwana unayo maneno ya uzima wa milele” (Zab 19). Maneno yanauwezo wakutufanya huru na kutuwekea matumaini mapya ndani yetu. Sheria ya Mungu, neno la Bwana, ni kamilifu na haki huburudisha nafsi, linatoa mwanga, ukweli na haki. Ni bora zaidi kuliko dhahabu. Ni matamu kuliko asali.
Mt. Paulo anawaambia Wakorintho, kwamba kusulubiwa kwa Kristo ni alama ya upendo wa Mungu kwetu. Alama ambayo hakuna anayetengwa. Lakini kwa Wayahudi ni kikwazo na kwa Wayunani ni ujinga. Wayahudi walikuwa wakitegemea upendo wa Mungu utokee moja kwa moja kama ulivyotokea katika Kitabu cha Kutoka walivyotoka Misri. Wayunani/Wagiriki hawakuamini kuhusu miujiza waliamini tu vitu kwa kutumia akili yao. Kifo cha Yesu msalabani hakiingii katika mantiki ya akili yao, na hivyo ilikuwa ni ujinga tu. Wengi wetu tunaweza kuanguka katika hali hizi. Kati ya Wagiriki au Wayahudi.
Wakati wa Pasaka, Yerusalemu ilikuwa imejawa na Wahujaji kutoka katika kila kona ya dunia. Walienda katika hekalu kusali, kutafuta ushauri kutoka kwa Makuhani, kutolea sadaka kwa Mungu, kutolea mapaji yao kwa Mungu kwa ukarimu, vitu ambavyo vingetumika tu kwenye hekalu. Hela ya Warumi ilioneakana kama hela isio na baraka hivyo ilibidi ibadilishwe na hela nyingine na wale wabadilisha fedha. Kipindi hiki wafanyabiashara walitumia muda huu kupata faida zaidi kuliko kipindi kingine chote cha Mwaka. Ni kipindi ambacho pia makuhani walipata faida sana. Waliruhusu wafanyabiashara na wabadilisha fedha kutumia hekalu. Sehemu yote ilijaa wahujaji wakifanya biashara mabali mbali. Sehemu ya sala imebadilishwa na makuhani wenyewe kuwa sehemu ya soko. Kipindi kiki cha Pasaka Yesu alikuja hekaluni. Yesu hakusema neno alifanyiza kiboko na kuwafukuza hekaluni. Kupindua meza zao , na njiwa kutolewa hekaluni. Yesu pia aliwatoa pia punda na kondoo njee.
Ishara hii ya Yesu, ilikuwa ni kukomesha dini ambayo ilibeba sadaka ya Wanyama. Kwa ushudhuda Yesu alikuja kwa upendo anaenda kutoa mwili wake mwenyewe, sadaka safi yenye kumpendeza Baba. “Hivi ndivyo tulivyotambua jinsi pendo lilivyo, kwamba Baba alimtoa Mwanae wa pekee, kwa ajili yetu” (1 Yn 3:16). Yesu aliyejitolea mwenyewe “mpole na mnyenyekevu wa moyo” (Mt 11:29), sasa anatoa amri: “Yatoeni haya, na acheni kuifanya nyumba ya Baba yangu kuwa pango la walanguzi” “hakutakuwa tena na biashara katika nyumba ya Mungu”(Zek 14:21). Kwa kufanya hivi Yesu alitangaza hali ya hatari ya kuchanganya dini na pesa, kumtumikia Mungu na mali. Hekima kubwa inahitajika hapa.
Kwaresima ni inatualika kutazama kwa karibu ndani yetu, parokia yetu, na kanisa letu. Je , mahekalu yetu yanafanana na mwili wa Yesu. Wayahudi walijifunga wenyewe na sheria ambazo hazikutoa sifa kwa Mungu. Kuabudu ni hali ya kweli ya kumwelekea Mungu pekee. Kuabudu inaleta maana sana kama utaweza kuishi kile unachofanya kanisani na kuweza kukifanya katika maisha ya kawaida. Kuabudu kwa kweli kunashikwa kwa kushika amri za Mungu, kuwajali jirani zetu na maskini, na kuwaheshimu watu wote na dunia, na kushirikisha kile ambacho tumepewa na Mungu na daima kuelewa kwamba tumetolewa katika utumwa, utumwa wa dhambi na hivyo tusimfanye mtu yeyote mtumwa kwasababu ya dhambi zetu na uovu wetu ndani yetu. Kumwabudu Mungu bila kuishi uaminifu na kuwa mtii kwa amri zake ni kumkosea heshima Mungu na kuonesha picha mbaya kuhusu Mungu.
Yesu alikuwa sahihi kabisa katika kulitunza na kulilinda hekalu la Mungu. Je, upo tayari kulilinda hekalu la Mungu? Na kumwambudu Mungu katika hali ya kweli na kumshuhudia katika hali zote? Yesu anaongea maneno ya Zaburi ya 69 “wivu wa nyumba yako hakika umenila”. Ni kitu ghani kinacho kumaliza wewe, Pesa, kazi, hofu, michezo, watoto, ndoa, umbea/kusengenya? Yesu anaongelea hekalu kama mwili wake mwenyewe. Je, ni namna gani unavyolitendea hakalu la mwili wako? Ni kwa jinsi gani unalitendea hekalu la ndugu yako? Unawatendeaje wagonjwa waliowekwa chini yako, wazee, yatima, na watu maskini?.
Sala: Bwana nisaidie nitengeneze njia zangu ili Yesu aweze kupata njia na sehemu ya kukaa ndani yangu. Amina
Copyright ©2013-2024 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com
No comments:
Post a Comment