NOVENA YA NOELI,
SIKU YA TANO
20 Desemba 2023
W: Bwana karibu atafika, Njoni kumwabudu.
K: Bwana karibu atafika, Njoni kumwabudu.
W: Furahi, ee binti Sion, na shangilia sana, ee binti Yerusalem! sikia,
Bwana atafika na siku ile utatokea mwanga mkuu, na milima itatonesha utamu; na
vi-lima vitatiririsha maziwa na asali, kwa sababu atafika nabii mkuu, na Yeye
atageuza Yerusalem.
K: Bwana karibu atafika, Njoni kumwabudu.
W: Sasa Mungu-Mtu wa nyumba ya Daudi atakuja kuketi juu ya kiti cha enzi,
mtamwona na moyo wenu utafurahi.
K: Bwana karibu atafika, Njoni kumwabudu
W: Sikia, atafika Bwana na Mlinzi wetu, Mtakatifu wa Israel. Kichwani mwake
ana taji la ufalme wake: atatawala nchi toka bahari mpaka bahari, toka mto
mpaka ukingoni mwa dunia.
K: Bwana karibu atafika, Njoni kumwabudu
Sikia, Bwana ataonekana, hadanganyi hata: akikawia mngoje, kwani atafika
tu, hawezi kuchelewa.
K: Bwana karibu atafika, Njoni kumwabudu
Bwana atashuka kama mvua juu ya ngozi yenye manyoya: katika siku zake
kutakuwa na haki na amani tele; na wafalme wote wa dunia watamwa-budu, na
makabila yote yatamtumikia.
K: Bwana karibu atafika, Njoni kumwabudu
Mtoto atazaliwa kwa ajili yetu na ataitwa Mungu mwenye nguvu: atakalia kiti
cha ezi cha Daudi baba yake; atatawala, na begani atachukua firhbo ya uwezo
wake.
K: Bwana karibu atafika, Njoni kumwabudu
Ee Bethlehem, mji wa Mungu mkuu, kwako atatokea Mtawala wa Israel: na uzazi
wake ni wa milele, atatukuzwa katika dunia yote; na atakapofika ita-kuwa amani
humu duniani mwetu.
K: Bwana karibu atafika, Njoni kumwabudu
ZABURI
Mbingu ifurahi nayo dunia ishangilie,
nanyi milima pigeni vigelegele.
Milima ionyeshe furaha,
na vilima vitoe haki.
Sababu Bwana wetu atafika,
na atawahurumia maskini wake.
Ee mbingu, nyesheni umande
na mawingu yatuletee
Mtakatifu, nchi ifunguke
na imzae mkombozi.
Utukumbuke, ee Bwana,
na utuletee wokovu wako.
Ee Bwana, utuonyeshe huruma yako,
nautupe ukombozi wako.
Ee Bwana, umlete Mwana - Kondoo mfalme wa dunia; atakayetawala toka jiwe la
jangwani mpaka mlima wa binti Sion.
Njoo utukomboe, ee Bwana, Mungu wa Majeshi:
utuonyeshe uso wako na tutaokoka.
Njoo, ee Bwana,
utuletee amani yako:
ili tufurahi
mbele yako kwa moyo safi.
Tupate kujua
njia yako humu duniani, ee Bwana:
na tujue wokovu
wako katika makabila yote.
Ee Bwana, amsha
nguvu zako na ufike:
ili utukomboe.
Njoo, ee Bwana,
usikawie:
uliondolee taifa
lako dhambi.
Ee, laiti
ungepasua mbingu na kushuka:
milima
ingeyeyuka mbele yako.
Njoo, ee Bwana,
utuonyeshe uso wako:
wewe unayeketi
juu ya Malaika.
Atukuzwe Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu
kama mwanzo na sasa na siku zote na milele. Amina.
WIMBO WA BIKIRA MARIA
K: Ee ufunguo wa Daudi na fimbo ya Israeli, unachofungua hapana awezaye
kufunga tena; unachofunga hapana awezaye kufungua. Njoo uwatoe mateka gerezani;
uwaangazie wale wanaokaa katika giza na katika kivuli cha mauti.
Moyo wangu wamtukuza Bwana,
Roho yangu inafurahi
kwa sababu ya Mungu Mwokozi wangu.
Kwa kuwa amemwangalia kwa huruma,
mtumishi wake mdogo,
Hivyo tangu sasa watu wote wataniita mwenye heri.
Kwa kuwa Mwenyezi Mungu amenitendea makuu,
jina lake ni takatifu.
Huruma yake kwa watu wanaomcha
hudumu kizazi hata kizazi.
Amefanya mambo makuu kwa mkono wake:
amewatawanya wenye kiburi katika mawazo ya mioyo yao;
amewashusha wenye nguvu kutoka vitu vyao vya enzi,
akawakweza wanyenyekevu.
Wenye njaa amewashibisha mema,
matajiri amewaacha waende mikono mitupu.
Amempokea Israeli mtumishi wake,
akikumbuka huruma yake.
Kama alivyowaahidia wazee wetu,
Abrahamu na uzao wake hata milele.
K: Ee ufunguo wa Daudi na fimbo ya Israeli, unachofungua hapana awezaye
kufunga tena; unachofunga hapana awezaye kufungua. Njoo uwatoe mateka gerezani;
uwaangazie wale wanaokaa katika giza na katika kivuli cha mauti.
Sala: Ee Bwana twakusihi uharikishe wala usichelewe na utuletee nguvu ya
juu, kusudi wote wanaotumainia huruma yako wapate kufariji wana majilio yako,
unayeishi na kutawala milele. Amina.
No comments:
Post a Comment