“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Jumatano, Novemba 1, 2023
Juma la 30 la Mwaka
SHEREHE YA WATAKATIFU WOTE
Uf 7:2-4, 9-14;
Zab 23:1-6;
1 Yn 3:1-3;
Mt 5:1-12
WATAKATIFU: WITO WA PAMOJA WA KUWA MTAKATIFU
Watakatifu ni wale walio jitahidi kuishi hapa duniani kadiri ya thamani ya
Injili. Hata baada ya kifo chao wanaendelea kuwa mfano na mashuhuda wa Injili
kwa wale waliobaki dunaini. Wakiwa wameumbwa wakiwa na mwili na damu kama sisi
walitamani kupata utakatifu. Hawa ni wale waliopata moyo kutoka kwa watakatifu
wengine wakisema “kama yeye amekuwa mtakatifu kwanini mimi nisiwe?” Watakatifu
mbinguni wana bahati ya kuwa mbele za Mungu daima. Walio wengi wakiwa bado hapa
duniani walifurahia kuwa ndani ya Mungu daima wakiwa hapa duaniani. Mbinguni ni
pale alipo Mungu, na Mungu yupo ndani ya mioyo yetu, kwahiyo walikuwa na Mungu
daima mbinguni. Watakatifu waliishi wakilijua hili na wakajikuta wakiwa katika
furaha ya Mungu daima.
Ingawaje wanafurahia maisha yao ya Mbinguni, bado wanahusiana na sisi. Mt.
Teresa wa Lisieux anasema vizuri kwamba “ninataka kuishi mbinguni huku
nikitenda matendo mema duniani" Watakatifu mbinguni wana kazi muhimu ya
kutuombea. Niwazi kwamba Mungu anafahamu mahitaji yetu, angeweza kutuambia sisi
tuende kwake moja kwa moja kwa sala zetu. Lakini ukweli ni kwamba Mungu
anapenda kutumia waombezi, na hivyo watakatifu wanakuwa waombezi wetu katika
maisha yetu. Anawatumia kuchukua sala zetu mbele Yake na hivyo kuturudishia
neema. Wanakuwa waombezi wakubwa wetu sisi kwa Mungu.
Watakatiu pia wanatupa sisi mfano wa utakatifu. Matendo ya ukarimu
walioishi duniani. Ushuhuda wa mapendo yao haikuwa kitendo cha wakati mmoja
katika historia. Bali ukarimu ni kuendelea kuishi na kuleta matokeo mazuri kwa
kuishi kwako. Hivyo ukarimu na maisha walio ishi watakatifu yanatupa kitu kwa
ajili ya maisha yetu. Ukarimu huu ni maisha yaliojenga muunganiko na sisi,
tunawapenda na kutaka kuishi kwa mfano wao. Hivyo kwa maombezi yao daima kuna
muunganiko wa mapendo kati yao na sisi.
Injili ya Leo inatualika kufuata zile heri kama njia ya kuelekea kupata
Utakatifu. Sisi ni nani tuishi maisha ya utakatifu? Mt. Augustino alijikuta
akipata ugumu wakuishi heri hizi, lakini alisoma maisha ya watakatifu na
akasema, “ Kama hawa watu wakawaida waume kwa wake waliweza, kwanini mimi
nisiweze?”
Katika somo la Injili Yesu anasema “heri Maskini wa roho, heri walio na
huzuni, heri wapole, heri walio na njaa na kiu ya kutenda haki, heri wenye
huruma, heri wenye moyo safi, heri wapatanishi, heri wenye kuonewa kwa aili ya
haki” lakini katika hali ya kawaida hizi sifa ni sifa za Yesu mwenyewe. Yeye
Yesu alikuwa, alikuwa mwenye moyo safi, mwenye huruma nk. Tunaposikia sauti
yake kila mtu kwa hali yake tumfuate tusifanye migumu ya mioyo yetu. Tumfuate
yeye tuweze kushiriki katika maisha yake. Kwani kwa Yesu kila kitu
kinawezekana. Atatufanya tuwe wakamilifu kama Baba wa mbinguni alivyo
mkamilifu.
Sala: Bwana, kama watakatifu wanavyo kuabudu mbinguni milele yote, ninaomba
kwa maombezi yao. watakatifu wa Mungu , mniombee. Niombeeni na mniletee neema
kutoka kwa Mungu niweze kuishi maisha ya mfano kama mlivyo ishi. Watakatifu
wote wa Mungu, mtuombee. Amina
No comments:
Post a Comment