MASOMO YA MISA NOVEMBA
8, 2023
JUMATANO, JUMA LA 31 LA
MWAKA
_____________
SOMO 1
Rum. 13:8-10
Msiwiwe na mtu chochote,
isipokuwa kupendana; kwa maana ampendaye mwenzake ameitimiza sheria. Maana kule
kusema, Usizini, Usiue, Usiibe, Usitamani, na ikiwapo amri nyingine yoyote,
inajumlishwa katika neno hili, ya kwamba, Mpende jirani yako kama nafsi yako.
Pendo halimfanyii jirani neno baya; basi pendo ndilo utimilifu wa sheria.
Neno la Bwana…
Tumshukuru Mungu.
_____________
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 112:1-2,4-5,9 (K)
(K) Heri atendaye
fadhili na kukopesha.
Aleluya,
Heri mtu yule amchaye
Bwana,
Apendezwaye sana na maagizo
yake.
Wazao wake watakuwa
hodari duniani;
Kizazi cha wenye adili
kitabarikiwa. (K)
Nuru huwazukia wenye
adili gizani;
Ana fadhili na huruma na
haki.
Heri atendaye fadhili na
kukopesha;
Atengenezaye mambo yake
kwa haki. (K)
Amekirimu, na kuwapa
maskini,
Haki yake yakaa milele,
Pembe yake itatukuzwa
kwa utukufu. (K)
_____________
SHANGILIO
Mt. 11:25
Aleluya, aleluya,
Nakushukuru, Baba, Bwana
wa mbingu nan chi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili,
ukawafunulia watoto wachanga.
Aleluya.
_____________
INJILI
Lk. 14:25-33
Makutano mengi
walipokuwa wakifuatana na Yesu, aligeuka, akawaambia, Kama mtu akija kwangu
naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake
waume kwa wake, na wanawe, na ndugu zake waume kwa wake; naam, na hata nafsi
yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu. Mtu yeyote asiyeuchukua msalaba
wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
Maana ni nani katika
ninyi, kama akitaka kujenga mnara, asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama, kwamba
anavyo vya kuumalizia? Asije akashindwa kuumaliza baada ya kuupiga msingi, watu
wote waonao wakaanza kumdhihaki, wakisema, Mtu huyu alianza kujenga, akawa hana
nguvu za kumaliza. Au kuna mfalme gani, akitaka kwenda kupigana na mfalme
mwingine, asiyeketi kwanza na kufanya shauri, kwamba yeye pamoja na watu elfu
kumi ataweza kukutana na yule anayekuja juu yake na watu elfu ishirini? Na kama
akiona hawezi, hutuma ujumbe kutaka sharti za Amani, mtu yule akali mbali.
Basi, kadhlika kila mmoja wenu asiyeacha vyote alivyo navyo, hawezi kuwa
mwanafunzi wangu.
Neno la Bwana… Sifa
kwako Ee Kristo.
_____________
Copyright © 2023,
"MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora –
Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see
www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment