Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

GHARAMA YA KUWA MFUASI!


“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya Kila siku
Jumatano, Novemba 8, 2023
Juma la 31 la Mwaka

Rom 13: 8-10;
Zab 112: 1-2, 4-5, 9 (K) 5; 
Lk 14: 25-33.


GHARAMA YA KUWA MFUASI!

Upendo ni amri kuu kuliko zote. Leo katika somo la kwanza Mt. Paulo anaelezea amri ya Yesu ya Upendo. Wayahudi walifahamu sheria na walikuwa wakijishughulisha kuzishika, mara nyingi huku wakisahau kitu chao muhimu. Ni msingi wa maisha ya Kikristo. Katika hali hii katika somo la kwanza Paulo anawaambia sheria zote zinafupishwa na sheria ya upendo. Upendo kwa Mungu na upendo kwa jirani. Kila mtu anayependa katika ukweli hawezi kukusudia kumuumiza mwenzie bali yupo tayari kujitoa sadaka kwa ajili yake. Mfuasi wa kweli ni yule aliye tayari kupenda. Mt. Mama Teresa wa Kalkuta alisema “kama mmoja anamuhukumu mtu hawezi kumpenda.” Hivyo hivyo mfuasi wa Kristo anapaswa kuwa na moyo uliojaa huruma licha ya moyo uliojaa hukumu juu ya kutimiza sheria. 

Katika injili ya Luka, tunaona Yesu yupo njiani kuelekea Yerusalemu. Ndani ya akili yake akiwa amejaa na kuhusu mateso, kifo na ufufuko ambavyo vingempata. Umati ulikuwa ukitembea pamoja naye lakini katika ukweli ulikuwa hautembei naye. Umati ulikuwa ukidhani kwamba Yesu amekuja kuwakomboa kutoka katika magonjwa, upungufu wa fedha na utawala wa Kirumi. Yesu anawakumbusha umati kitu ambacho kinahitajika ili waweze kutembea naye katika hali ya ukweli na mafanikio. Anawaambia kwamba ufuasi sio kazi rahisi ya kuomba. Kumfuata yeye inampasa mmoja kuacha ndugu hata wa familia na kumfuata, baba, mama, mwenzi wa ndoa, watoto nk. Kwa maneno mengine kumfuata Yesu tunapaswa tumuweke wa kwanza zaidi ya kitu kingine. 

Yesu anaelezea mambo matatu katika ufuasi: kuachana na kujishika na familia, kukutana na kujikatalia binafsi na kuachia mali. Anawaalika wale wote ambao watamfuata yeye waweze kukubali na kutopata heshima na kupata mateso. Mfuasi kamili wa Yesu hatafuti faraja, kufarijiwa na marafiki, wala kubakiza maisha yake. Hivyo ufuasi sio rahisi, kuna gharama isio isha. Je, mimi na wewe tupo tayari kulipa gharama hiyo? 

Sala: Bwana Yesu, nisaidie niweze kuona vile vitu vyote vinavyo nizuia mimi nishindwe kukupenda wewe. Nikiwa ninatambua kitu ambacho kinanitoa kwenye Imani, nipe ujasiri niweze kukuchagua wewe zaidi ya kitu kingine. Nipe hekima niweze kutambua ni kwa jinsi ghani naweza kukuchagua wewe zaidi ya kitu chochote. Yesu, nakuamini wewe. Amina


Copyright ©2013-2023 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com

No comments:

Post a Comment