MASOMO YA MISA NOVEMBA
7, 2023
JUMANNE, JUMA LA 31 LA
MWAKA
_____________
SOMO 1
Rum. 12:5-16
Sisi tulio wengi tu
mwili mmoja katika Kristo, na viungo, kila mmoja kwa mwenzake. Basi kwa kuwa
tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema tuliyopewa; ikiwa unabii,
tutoe unabii kwa kadiri ya Imani; ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu;
mwenye kufundisha, katika kuonya kwake; mwenye kukirimu, kwa moyo mweupe;
mwenye kusimamia, kwa bidi; mwenye kurehemu, kwa furaha.
Pendo na lisiwe na
unafiki; lichukieni lililo ovu, mkiambatana na lililo jema. Kwa pendo la udugu,
mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu; kwa bidii, si
walegevu; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia Bwana; kwa tumaini,
mkifurahi; katika dhiki, mkisubiri; katika kusali, mkidumu; kwa mahitaji ya
watakatifu, mkifuata ukarimu; katika kukaribisha wageni, mkijitahidi.
Wabarikini wanaowaudhi;
barikini, wala msilaani. Furahini pamoja nao wafurahio; lieni pamoja nao
waliao. Mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi. Msinie yaliyo makuu, lakini mkubali
kushughulishwa na mambo manyonge.
Neno la Bwana…
Tumshukuru Mungu.
_____________
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 131
(K) Moyo wangu uwe na
Amani kwako, Ee Bwana.
Bwana, moyo wangu hauna
kiburi,
Wala macho yangu
hayainuki.
Wala sijishughulishi na
mambo makuu,
Wala na mambo yashindayo
nguvu zangu. (K)
Hakika nimeituliza nafsi
yangu,
Na kuinyamazisha.
Kama mtoto aliyeachishwa
Kifuani mwa mama yake;
Ndivyo roho yangu ilivyo
kwangu. (K)
Ee Israeli, umtarajie
Bwana,
Tangu leo n ahata
milele. (K)
_____________
SHANGILIO
Zab. 147:12,15
Aleluya, aleluya,
Msifu Bwana, Ee
Yerusalemu, huipeleka amri yake juu ya nchi.
Aleluya.
_____________
INJILI
Lk. 14:15-24
Mmojawapo wa wale
walioketi chakulani pamoja na Yesu alimwambia, Heri yule atakayekula mkate
katika ufalme wa Mungu. Akamwambia, Mtu mmoja alifanya karamu kubwa, akaalika
watu wengi, akamtuma mtumwa wake saa ya chakula awaambie wale walioalikwa,
Njoni, kwa kuwa vitu vyote vimekwisha kuwekwa tayari. Wakaanza wote kutoa
udhuru kwa nia moja. Wa kwanza alimwambia, Nimenunua shamba, sharti niende
nikalitazame; tafadhali unisamehe. Mwingine akasema, Nimenunua ng’ombe jozi
tano, ninakwenda kuwajaribu; tafadhali unisamehe. Mwingine akasema, Nimeoa mke,
na kwa sababu hiyo siwezi kuja.
Yule mtumwa akaenda,
akampa bwana wake habari ya mambo hayo. Basi, yule mwenye nyumba akakasirika,
akamwambia mtumwa wake, Toka upesi, uende katika njia kuu na vichochoro vya
miji, ukawalete hapa maskini, na vilema, na vipofu, na viwete. Mtumwa akasema,
Bwana, hayo uliyoagiza yamekwisha tendeka, n ahata sasa ingaliko nafasi.
Bwana akamwambia mtumwa,
Toka nje uende barabarani na mipakani, ukawashurutishe kuingia ndani, nyumba
yangu ipate kujaa. Maana nawaambia ya kwamba katika wale walioalikwa, hapana
hata mmoja atakayeionja karamu yangu.
Neno la Bwana… Sifa
kwako Ee Kristu.
_____________
Copyright © 2023,
"MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora –
Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment