MASOMO YA MISA NOVEMBA
4, 2023
JUMAMOSI JUMA LA 30 LA
MWAKA
KUMBUKUMBU YA MT. KAROLI
BOROMEO
_____________
SOMO 1
Rum. 11:1-2, 11-12,
25-29
Nauliza. Je! Mungu
aliwasukumia mbali watu wake? Hasha! Kwa kuwa mimi nami ni Mwisraeli, mmoja wa
wazao wa Ibrahimu, mtu wa kabila ya Benyamini. Mungu hakuwasukumia mbali watu
wake aliowajua tokea awali.
Basi nasema, Je!
Wamejikwaa hata waanguke kabisa? Hasha! Lakini kwa kosa lao wokovu umewafikilia
Mataifa, ili wao wenyewe watiwe wivu. Basi, ikiwa kosa lao limekuwa utajiri wa
ulimwengu, na upungufu wao umekuwa utajiri wa Mataifa, je! Si Zaidi sana
utimilifu wao?
Kwa maana, ndugu zangu,
sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu
ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili. Hivyo Israeli wote
wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo
na maasia yakee. Na hili ndilo agano langu nao, Nitakapowaondolea dhambi zao.
Basi kwa habari ya
Injili wamekuwa adui kwa ajili yenu; bali kwa habari ya kule kuchaguliwa
wamekuwa wapenzi kwa ajili ya baba zetu. Kwa sababu karama za Mungu hazina
majuto, wala mwito wake.
Neno la Bwana…
Tumshukuru Mungu.
_____________
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 94:12-15,17-18 (K)
16
(K) Bwana hatawatupa
watu wake.
Ee Bwana, heri mtu yule
umwadhibuye,
Na kumfundisha kwa
sheria yako;
Upate kustarehesha siku
za mabaya,
Hata asiye haki
atakapochimbiwa shimo. (K)
Kwa kuwa Bwana
hatawatupa watu wake,
Wala hutauacha urithi
wake,
Maana hukumu itairejea
haki,
Na wote walio wanyofu wa
moyo wataifuata. (K)
Kama Bwana asingalikuwa
msaada wangu,
Nafsi yangu kwa upesi
ingalikaa penye kimya.
Niliposema, Mguu wangu
unateleza;
Ee Bwana, fadhili zako
zilinitegemeza. (K)
_____________
SHANGILIO
Zab. 119:135
Aleluya, aleluya,
Umwangazie mtumishi wako
uso wako, na kunifundisha amri zako.
Aleluya.
_____________
INJILI
Lk. 14:1, 7-11
Yesu alipoingia ndani ya
nyumba ya mtu mmoja miongoni mwa wakuu wa Mafarisayo siku ya sabato, ale
chakula, walikuwa wakimvizia.
Akawaambia mfano wale
walioalikwa, alipoona jinsi walivyochagua viti vya mbele; akisema, Ukialikwa na
mtu arusini, usiketi katika kiti cha mbele; isiwe kwamba amealikwa mtu mwenye
kustahiwa kuliko wewe, akaja yule aliyewaalika wewe na yeye, na kukuambia,
Mpishe huyu! Ndipo utakapoanza kwa haya kushika mahali pa nyuma, ili ajapo yule
aliyekualika akuambie, Rafiki yangu, njoo huku mbele Zaidi; ndipo utakapokuwa
na utukufu mbele ya wote walioketi pamoja nawe. Kwa maana kila ajikwezaye
atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa.
Neno la Bwana… Sifa
kwako Ee Kristo.
_____________
Copyright © 2023,
"MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora –
Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see
www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment