“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Jumamosi, Novemba 4, 2023
Juma la 30 la Mwaka
Kumbukumbu ya Mt. Karoli Boromeo, Askofu.
Rom 11: 1-2, 11-12, 25-29;
Zab 94: 12-15, 17-18 (K) 14;
Lk 14: 1, 7-11.
HATARI YA MAJIVUNO
Kila mwanadamu anatamani kuwa mtu maarufu. Tunakazana kuheshimiwa na
kutambuliwa na watu. Lakini jitihada hizi za mtu zinaweza kumuangusha. Katika
somo la kwanza la Mtume Paulo kwa Warumi, Paulo anazunguzia juu ya upofu wa
mafarisayo na Waandishi, walikuwa wataalamu wa maandiko na sheria lakini kwa
sababu ya majivuno yao wakashindwa kumtambua Masiha ambaye Maandiko
yamemuongelea. Katika hali zetu za anasa, kutafuta mamlaka, tunakuwa na hali ya
kusahau sisi ni akina nani. Viongozi wazuri wanaanza kuwa wadhulumu kwa njia ya
kukosa haki. Unyenyekevu kwa njia nyingine ni kutambua sisi ni akina nani. Na
unaaza kwa kutambua kuwa Mungu ni chanzo la lengo la maisha. Hivyo nikutumia
vipaji vyetu vyote, vile ambavyo vinatutambulisha na Mungu, kumpa yeye utukufu
na kuwasaidia ndugu zetu, kaka na dada zetu.
Yesu kwa kutoa mfano wa karumu ya harusi, moja kwa moja aliwaongelea wale
waliokuwa naye mizani wakila, katika nyumba ya Farisayo. Bilashaka wale
waliokuwa wakimsikiliza waliguswa na hali zao za kujitazama wao wenyewe na
kushindwa kuwatazama wengine. Itakuwa ni jambo la aibu na kuaibishwa wakati
umekaribishwa viti vya mbele alafu baadae wanakushusha na kukuweka katika
sehemu ya mwisho. Aibu hii ni kwa wale waliokamatwa na anasa za ulimwengu. Yesu
alitumia mfano huu kwa kuonesha hatari ya kuishi katika hali hiyo ya majivuno.
Anaendelea kusema “kwa yeye yule ambaye atajikweza atashushwa, lakini yule
ambaye atajishusha atakwezwa”.
Tunapaswa tuchuguze dhamiri zetu kila siku juu ya majivuno. Majivuno
yanachukuliwa daima kama “mama wa dhambi zote” kutokana na sababu. Majivuno
yanapelekea utendaji wa dhambi nyingine katika namna mbali mbali, ni chanzo cha
dhambi nyingine zote. Hivyo kama tunatamani kuwa wakamilifu katika maisha ni
vizuri kukimbilia unyenyekevu wa kweli siku zote. Unyenyekevu si kitu kingine
zaidi ya kuyaona mambo kama yalivyo. Mtu mnyenyekevu anajiona mwenyewe katika
ukweli wa Kimungu. Hili ni ngumu kulifanya kwasababu inatubidi sisi kujiona na
kuutazama udhaifu wetu na kwamba Mungu ndiye tegemezi letu. Tunaweza kufanya
mambo mengi ulimwenguni kwa kutumia nguvu zetu wenyewe. Lakini hatuwezi kupata
furaha ya kweli mpaka tumefungua mioyo yetu katika hali ya kweli na kumtegemea
Mungu kwa kila kitu. Unyenyekevu unatusaidia kuosha mioyo yetu kutoka katika
kitu kigumu ambacho tumeshindwa kukitoa rohoni mwetu. Tujichunguze leo ni kwa
jinsi ghani tulivyo huru kutoka katika majivuno yetu? Tutembee katika njia ya
unyenyekevu ndugu yangu.
Sala: Bwana, nifanye mimi niwe mnyenyekevu. Safisha kabisa majivuno katika
maisha yangu ili niweze kukujeukia wewe na wewe pekee. Yesu nakuamini wewe.
Amina
No comments:
Post a Comment