MASOMO YA MISA, NOVEMBA
2, 2023
ALHAMISI JUMA LA 30 LA
MWAKA
KUWAKUMBUKA MAREHEMU
WOTE
(Masomo haya na zaburi
yamechaguliwa kutoka masomo mengine mengi ya siku ya leo.)
SOMO 1
Isa 25: 6-9
Na katika mlima huu
Bwana wa majeshi atawafanyia mataifa yote karamu ya vitu vinono, karamu ya
divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, karamu ya vinono vilivyojaa mafuta,
karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, iliyochujwa sana. Naye katika
mlima huu atauharibu uso wa sitara iliyowekwa juu ya watu wote, na utaji ule
uliotandwa juu ya mataifa yote. Amemeza mauti hata milele; na Bwana Mungu
atafuta machozi katika nyuso zote; na aibu ya watu wake ataiondoa katika
ulimwengu wote; maana Bwana amenena hayo. Katika siku hiyo watasema,Tazama,
huyu ndiye Mungu wetu, Ndiye tuliyemngoja atusaidiye; Huyu ndiye Bwana
tuliyemngoja, Na tushangilie na kuufurahia wokovu wake.
Neno la Bwana…
Tumshukuru Mungu
_____________
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 23 (K) 1 au 4
(K. 1) Bwana ndiye mchungaji
wangu, sitapungukiwa na kitu. (au)
(K. 4) Nijapopita kati
ya bonde la uvuli wa mauti, sitaogopa mabaya;
Kwa maana wewe upo pamoja nami
Bwana ndiye mchungaji
wangu,
Sitapungukiwa na kitu.
Katika malisho ya majani
mabichi hunilaza.
Kando ya maji ya utulivu
huniongoza. (K)
Hunihuisha nafsi yangu;
na kuniongoza,
Katika njia za haki kwa
ajili ya jjina lake.
Naam, nijapopita kati ya
bonde la uvuli wa mauti,
Sitaogopa mabaya;
Kwa maana wewe upo
pamoja nami,
Gongo lako na fimbo
yangu vyanifariji. (K)
Waandaa meza mbele
yangu,
Machoni pa watesi wangu.
Umenipaka mafuta
kichwani pangu,
Na kikombe changu
kinafurika. (K)
Hakika wema na fadhili
zitanifuata,
Siku zote za maisha
yangu;
Nami nitakaa nyumbani
mwa Bwana milele. (K)
_____________
SOMO 2
Rum 5:5-11
Tumaini halitahayarishi;
kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho
Mtakatifu tuliyepewa sisi. Kwa maana hapo tulipokuwa hatuna nguvu, wakati
ulipotimia, Kristo alikufa kwa ajili ya waovu. Kwa kuwa ni shida mtu kufa kwa
ajili ya mtu mwenye haki; lakini yawezekana mtu kuthubutu kufa kwa ajili ya mtu
aliye mwema. Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa
Kristo alikuwa kwa ajili yetu, tulipokwa tungali wenye dhambi. Basi zaidi sana
tukiisha kuhesabiwa haki katika damu yake, tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye.
Kwa maana ikiwa tulipokuwa adui tulipatanishwa na Mungu kwa mauti ya Mwana
wake; zaidi sana baada ya kupatanishwa tutaokolewa katika uzima wake. Wala si
hivyo tu, ila pia twajifurahisha katika Mungu kwa Bwana wetu Yesu Kristo,
ambaye kwa yeye sasa tumeupokea huo upatanisho.
Neno la Bwana…
Tumshukuru Mungu
_____________
SHANGILIO
Ufu. 14:13
Aleluya, aleluya,
Heri wafu wafao katika
Bwana tangu sasa! Wapate kupumzika baada ya taabu zao, kwa kuwa matendo yao
yafuatana nao.
Aleluya.
_____________
INJILI
Mk 15: 33-39, 16: 1-6.
Ilipokuwa saa sita,
palikuwa na giza juu ya nchi yote, hata saa tisa. Na saa tisa Yesu akapaza
sauti yake kwa nguvu, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Maana yake, Mungu wangu,
Mungu wangu, mbona
umeniacha? Na baadhi yao
waliosimama pale, walisema, Tazama, anamwita Eliya. Na mmoja akaenda mbio,
akajaza sifongo siki, akaitia juu ya mwanzi, akamnywesha, akisema, Acheni; na
tuone kwamba Eliya anakuja kumtelemsha. Naye Yesu akatoa sauti kuu, akakata roho.
Pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini. Basi yule akida,
aliyesimama hapo akimwelekea, alipoona ya kuwa alikata roho jinsi hii, akasema,
Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu.
Hata sabato ilipokwisha
kupita, Mariamu Magdalene na Mariamu mamaye Yakobo, na Salome walinunua
manukato wapate kwenda kumpaka. Hata alfajiri mapema, siku ya kwanza ya juma,
wakaenda kaburini, jua lilipoanza kuchomoza.
Wakasemezana wao kwa
wao, Ni nani atakaye-vingirisliia lile jiwe mlangoni pa kaburi? Hata
waalipotazama, waliona ya kuwa lile jiwe limekwisha kuvingirishwa; nalo
lilikuwa kubwa mno. Wakaingia kaburini wakaona kijana ameketi upande wa kuume,
amevaa vazi jeupe; wakastaajabu. Naye akawaambia, Msistaajabu; mnamtafuta Yesu
Mnazareti, aliyesulibiwa; amefufuka; hayupo hapa; patazameni mahali
walipomweka.
Neno la Bwana... Sifa
kwako Ee Kristo.
_____________
Copyright © 2023, "MASOMO
YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings
reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment