MASOMO YA MISA, NOVEMBA
19, 2023
DOMINIKA YA 33 YA MWAKA
A WA KANISA
_____________
MWANZO:
Yer. 29:11, 12, 14
Bwana asema: Mawazo
ninayowawazia ninyi ni mawazo ya amani wala si ya mabaya. Nanyi mtaniita nami
nitawasikiliza, nami nitawarudisha kutoka mahali pote watu wenu waliofungwa.
_____________
SOMO 1
Mit. 31:10-13, 19-20,
30-31
Mke mwema, ni nani
awezaye kumwona?
Maana kima chake chapita
kima cha marijani.
Moyo wa mumewe
humwamini, Wala hatakosa kupata mapato.
Humtendea mema wala si
mabaya, siku zote za maisha yake.
Hutafuta sufu na kitani;
taaa yake haizimiki usiku.
Hutia mikono yake katika
kusokota; na mikono yake huishika pia.
Huwakunjulia maskini
mikono yake;
Naam, huwanyoshea
wahitaji mikono yake.
Upendeleo hudanganya, na
uzuri ni ubatili; bali mwanamke amchaye Bwana, ndiye atakayesifiwa.
Mpe mapato ya mikono
yake, na matendo yamsifu malangoni.
Neno la Bwana… Tumshukuru
Mungu.
____________
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 128:1-5 (K)1
(K) Taabu ya mikono yako
hakika utaila.
Heri kila mtu amchaye
Bwana,
Aendaye katika njia
yake.
Heri yao wale wamchao
Bwana,
Utakuwa mwenye heri na
Baraka tele. (K)
Mkeo atakuwa kama
mzabibu uzaao,
Vyumbani mwa nyumba
yako.
Wanao kama miche ya
mizeituni,
Wakiizunguka meza yao.
(K)
Tazama, atabarikiwa
hivyo, yule amchaye Bwana,
Bwana akubariki toka
Sayuni,
Uone uheri wa Yerusalemu
Siku zote za maisha
yako. (K)
_____________
SOMO 2
1The. 5:1-6
Ndugu zangu, kwa habari
ya nyakati na majira, hamna haja niwaandikie. Maana ninyi wenyewe mnajua yakini
ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku. Wkati wasemapo. Kuna
amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu
umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa. Bali ninyi, ndugu, hammo
gizani, hata siku ile iwapate kama mwivi. Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa
nuru, na wana wa mchana; sisi si wa usiku, wala wa giza. Basi tusilale usingizi
kama wengine, bali tukeshe, na kuwa na kiasi.
Neno la Bwana…
Tumshukuru Mungu.
_____________
SHANGILIO
Mt. 24:42, 44
Aleluya, aleluya,
Kesheni basin a kujiweka
tayari, kwa maana hamjui saa atakayokuja, Mwana wa Adamu.
Aleluya.
_____________
INJILI
Mt. 25:14 – 30
Ufalme wa mbinguni
utafanana na mtu atakaye kusafiri, akawaita watumwa wake, akaweka kwao mali
zake. Akampa mmoja talanta tano, na mmoja talanta mbili, na mmoja talanta moja;
kila mtu kwa kadiri ya uwezo wake; akasafiri. Mara yule aliyepokea talanta tano
akaenda, akafanya biashara nazo, akachuma faida talanta nyingine tano. Vile
vile na yule mwenye mbili, yeye naye akachuma nyingine mbili faida. Lakini yule
aliyepokea moja alikwenda akafukua chini, akaificha fedha ya bwana wake. Baada
ya siku nyingi akaja bwana wa watumwa wale, akafanya hesabu nao. Akaja yule
aliyepokea talanta tano, akaleta talanta nyingine tano, akisema, Bwana, uliweka
kwangu talanta tano, tazama talanta nyingine tano nilizopata faida. Bwana wake
akamwambia, Vema, mtumwa mwema na uaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache,
nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako. Akaja na yule
aliyepokea talanta mbili, akasema, Bwana, uliweka kwangu talanta mbili, tazama,
talanta nyingine mbili nilizopata faida. Bwana wake akamwambia, Vema mtumwa
mwema na uaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi;
ingia katika furaha ya bwana wakeo. Akaja na yule aliyepokea talanta moja,
akasema, Bwana, nalitambua ya kuwa wewe u mtu mgumu, wavuna usipopanda,
wakusanya usipotawanya; bali nikaogopa, nikaenda nikaificha talanta yako katika
ardhi; tazama, unayo iliyo yako. Bwana wake akajibu, akamwambia, Wewe mtumwa
mbaya na ulegevu, ulijua ya kuwa navuna nisipopanda, nakusanya nisipotawanya;
basi, ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoao riba; nami nikija ningalipata
iliyo yangu na faida yake. Basi mnyang’anyeni talanta hiyo, mpeni yule aliye
nazo talanta kumi. Kwa maana kila mwenye kitu atapewa, na kuongezewa tele,
lakini asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang’anywa. Na mtumwa yule
asiyefaa, mtupeni mbali katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga
meno.
Neno la Bwana… Sifa
kwako Ee Kristo.
_____________
Copyright © 2023,
"MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora –
Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see
www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment