Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

KUVUMILIA UKIWA KATIKA SALA!


“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Jumamosi, Novemba 18, 2023
Juma la 32 la Mwaka

Jumamosi kumbukumbu ya Bikira Maria

Hek 18: 14-16; 19: 6-9;
Zab 105: 2-3, 36-37, 42, 43; 
Lk 18: 1-8.


KUVUMILIA UKIWA KATIKA SALA! 

Sala inaweza kufanya miujiza. Wala hakuna wasi wasi kuhusu hili, lakini je, mtu atawezaje kusali daima? Kitu ambacho Yesu anahitaji kutoka kwetu ni kuvumilia kwetu katika imani yetu, kuwa na Mungu daima hata pale ambapo mambo yanaenda kinyume na matazamio yetu na kuwa magumu. Hili linawezekana kama tutamruhusu Mungu awe dereva wa amaisha yetu. Yesu ametuonesha sisi njia. Yeye alikuwa daima na mawasiliano na Baba yake katika sala, kuanzia mwanzoni mpaka mwisho. Alifahamu kabisa Baba hawezi kumuacha. 

Katika Injili ya leo, Yesu anatueleza habari ambayo ni kweli kabisa, kuhusu mjane ambaye hakuchoka kumsumbua kadhi dhalimu mpaka alivyompa haki yake. Kuvumilia kunalipa, na hili ni kweli kabisa na hasa kwa wale wanaomwamini Mungu. Yesu anatuelezea ni kwajinsi ghani Mungu alivyo mwepesi wakutuletea haki yake, baraka na msaada tunapo muhitaji. Lakini tunaweza kukata tamaa haraka na kuwa na mioyo hafifu katika kumwomba Baba yetu wa Mbinguni neema zake na msaada. Yesu anawapa matumaini mapya na ujasiri wafuasi wake.

 Katika maisha ya sasa, tunaweza kukumbana na matatizo makubwa sana na majaribu na magumu mengi lakini hatupaswi kupoteza tumaini la kumwamini Mungu. Hukumu ya mwisho itafunua kwamba haki ya Mungu itakuwa juu ya wasio haki yaliyotendwa na viumbe vyake. Yesu anamalizia kwa swali lakujiuliza sisi, je mimi na wewe tunaimani, Imani inayovumilia mpaka mwisho?  

Sala: Bwana, nisaidie mimi nikuamini na kukutafuta wewe daima bila kuchoka. Amina



Copyright ©2013-2017 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.

No comments:

Post a Comment