MASOMO YA MISA, NOVEMBA
12, 2023
DOMINIKA YA 32 YA MWAKA
MWANZO:
Zab. 88:2
Maombi yangu yafike
mbele zako, uutegee ukulele wangu sikio lako, Ee Bwana.
_____________
SOMO 1
Hek. 6:12-16
Hekima hung’aa, wala
hafifii;
Huonekana upesi nao
wampendao;
Hupatikana nao
wamtafutao.
Hutangulia kujionyesha
kwao wamtakao,
Amtafutaye mapema hana
kazi ngumu;
Atamkuta ameketi
mlangoni pake.
Kumtia fikirani ni
ufahamu mkamilifu;
Naye mwenye kukesha kwa
ajili yake
Atakuwa mara hana
masumbufu.
Yeye huzunguka-zunguka
mwenyewe,
Akiwatafuta wao
wanaomstahili;
Njiani hujidhihirisha
kwao kwa upendo,
Hukutana nao katika kila
kusudi.
Neno la Bwana…
Tumshukuru Mungu.
_____________
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 63:1-7 (K) 1
(K) Ee Mungu, Mungu
wangu, nafsi yangu inakuonea kiu.
Ee Mungu, Mungu wangu
nitakutafuta mapema,
Nafsi yangu inakuonea
kiu.
Mwili wangu wakuonea
shauku,
Katika nchi kama na
uchovu, isiyo na maji. (K)
Ndivyo nilivyokutazama
katika patakatifu,
Nizione nguvu zako na
utukufu wako.
Maana fadhili zako ni
njema kuliko uhai,
Midomo yangu itakusifu.
(K)
Ndivyo nitakavyokubariki
maadamu ni hai,
Kwa jina lako nitainua
mikono yangu.
Nafsi yangu itakinai
kama kushiba mafuta na vinono,
Kinywa changu kitakusifu
kwa midomo ya furaha. (K)
Ninapokukumbuka
kitandani mwangu,
Nakutafakari Wewe
makesha yote ya usiku.
Maana Wewe umekuwa
msaada wangu,
Na uvulini mwa mbawa
zako nitashangilia. (K)
_____________
SOMO 2
1Thes. 4:13-18
Ndugu, hatutaki msijue
habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na
matumaini. Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo
na hao waliolala katika yesu, Mungu atawaleta pamoja naye. Kwa kuwa twaambieni
haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja
kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti. Kwa sababu Bwana
mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu,
na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha
sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili
tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele. Basi,
farijianeni kwa maneno hayo.
Neno la Bwana…
Tumshukuru Mungu.
_____________
SHANGILIO
Yn. 14:23
Aleluya, aleluya,
Mtu akinipenda
atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda, nasi tutakuja kwake.
Aleluya.
_____________
INJILI
Mt. 25:1-13
Yesu aliwaambia
wanafunzi wake: Ufalme wa mbinguni utakapofanana na wanawali kumi, waliotwaa
taa zao, wakatoka kwenda kumlaki bwana arusi. Watano wao walikuwa wapumbavu, na
watano wenye busara. Wale waliokuwa wapumbavu walizitwaa taa zao, wasitwae na
mafuta pamoja nao; bali wale wenye busara walitwaa mafuta katika vyombo vyao
pamoja na taa zao. Hata bwana arusi alipokawia, wote wakasinzia wakalala
usingizi. Lakini usiku wa manane, pakawa na kelele, Haya, bwana arusi, tokeni
mwende kumlaki. Mara wakaondoka wanawali wale wote, wakazingeneza taa zo. Wale
wapumbavu wakawaambia wenye busara, Tupeni mafuta yenu kidogo; maana taa zetu
zinazimika. Lakini wale wenye busara wakawajibu, wakisema, Sivyo; hayatatutosha
sisi na ninyi; afadhali shikeni njia mwende kwa wauzao, mkajinunulie. Na hao
waliokuwa wakienda kununua, bwana arusi akaja, nao waliokuwa tayari wakaingia
pamoja naye arusini; mlango ukafungwa. Halafu wakaja na wale wanawali wengine,
wakasema, Bwana, Bwana, utufungulie. Akajibu akasema, Amin, nawaambia, siwajui
ninyi. Basi kesheni, kwa sababu hamwijui siku wala saa.
Neno la Bwana… Sifa
kwako Ee Kristo.
_____________
Copyright © 2023,
"MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora –
Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see
www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment