“ASALI ITOKAYO MWMABANI”
Tafakari ya kila siku
Jumamosi, Novemba 11, 2023
Juma la 31 la Mwaka
Kumbukumbu ya Mt. Martini wa Tours
Rom 16:3-9, 16, 22-27;
Zab 144:2-5, 10-11;
Lk 16: 9-15.
KUVUNJIKA KWA UKWELI WA NAFSI ZETU
Kuja kwa mitandao ya kijamii, huku ikileta mafanikio makubwa, imeleta pia
kitu tunachoweza kukiita “HKM” (Hofu ya Kukosa Matukio). Tangu simu za
“smartphones” ziingie zimerahisisha mawasiliano katika kazi kila mara. Lakini
zimeleta pia “hofu ya kukosa matukio” “HKM”. Hili linawafanya watu kila mara
awe anatazama simu yake ili asipitwe, kuangalia ujumbe, facebook, hata wakati
mwingine kuchati wakati wakiwa wanakula mlo wa pamoja nyumbani au wakiwa
wamehudhuria sherehe ya kuzaliwa ya rafiki nk. Wakati mwingine tunakuwa na hofu
juu ya uchaguzi waliochagua watu wengine. Je, kuna mwingine amenunua simu mpya?
Ni iphone au ni ipad? Je, rafiki yangu atapa hoteli ya kisasa yenye kuvutia?
Je, atapata mtu wakumtengenezea nguo zuri?
Tunajisikia vizuri baada tu ya kusoma ujumbe wa wenzetu kutoka facebook,
nakujiuliza kuna tukio limenipita kweli? Hali hii na hamu hii ambayo
inawaathiri watu 4 kati ya kumi kila siku, inatuonesha sisi hofu tulio nayo
kuhusu wengine, tuna mashaka kweli kwa vitu ambavyo hatuna na tunakosa vile
ambavyo tunavyo sisi wenyewe. Sisi pia tunapenda sana vitu vyetu vipokee sifa
kwa wengine, na kama hatujapata sifa tunaumia kweli.
Je, una hofu zaidi ya watu kuhusu maisha yako au hofu ya nini Mungu anawaza
juu yako? ‘Mungu anafahamu moyo’ anafahamu sisi ni wanani kutoka ndani. Mara
nyingi sisi tunahangaika sana kuhusu hofu yetu juu ya watu wanawaza nini kuhusu
mimi. Injili ya leo inaenda ndani katika mioyo ya Mafarisayo, wao walikuwa na
hali ya kuogopa sana wanaonekana je machoni pa watu, na kusahau, Mungu
anawaonaje mioyoni mwao. Wakati mwingine kama Mafarisayo sisi nasi tunakazana
sana kutaka kuonekana vizuri machoni pa watu, wakati huo huo Mungu anafahamu
undani wa mioyo yetu na anajua sivyo ilivyo. Wakati mwingine watu wanaweza kuwa
na picha tofauti juu yetu, kitu ambacho kinaweza kutufanya sisi pia tuumie.
Wakati haya yanatokea tunaweza kushikwa na hasira na kuanza kujisafisha na hata
kuwachukia wengine. Lakini katika hili ni kipi kilicho cha muhimu? Sisi
tunapaswa kuwa na hofu ya nini? Ukweli ni kwmaba tunapaswa kuwa na hofu ya
jinsi Mungu anavyo tuona sio kuogopa yale yasio ya muhimu. Tafakari juu ya hali
yako ya kuogopa maneno ya watu kuliko dhambi unazo mtendea Mungu. Tambua Mungu
anataka uishi maisha ya kweli ya jinsi unavyo jiweka mbele za watu. Ogopa tu
kila ambacho Mungu anajua juu yako, mambo mengine mwachie yeye. Mwisho wa vyote
hilo ndilo la muhimu.
Sala: Bwana, nisaidie niweze kuona kile ambacho kipo ndani ya moyo wako na
niweze kujishughulisha na jinsi unavyo niona mimi. Yesu nakuamini wewe. Amina
Copyright ©2013-2023 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki:
see www.fur-kat.blogspot.com
No comments:
Post a Comment