“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Jumatano, Oktoba 25, 2023
Juma la 29 la Mwaka
Rom 6: 12-18;
Zab 124: 1-8 (K) 8;
Lk 12: 39-48.
UFUASI: WITO WA KUWA MWAMINIFU, SI KUFANIKIWA!
Uaminifu na ukweli ni mambo makuu matakatifu na mazuri kabisa yaliowekwa
kama zawadi katika akili ya mwanadamu. Kuwa mwaminifu katika mambo madogo sana
ni njia ya kuelewa, kuboresha, na kuelezea nguvu itakiwayo kutenda mambo
makubwa. Uaminifu si kutenda mambo sahihi mara moja tu nakuacha, bali kufanya
mambo sahihi mara zote na zaidi ya kawaida. Mfano katika Injili unatutaka sisi
kuwa tayari, kuwa waaminifu kila wakati, tutende mema na kuwa waaminifu si
kwasababu tunaogopa siku ya mwisho bali tutende wema na kuwa waaminifu kwani
ndio tabia ya Kimungu.
Je, kadiri ya Yesu nini maana ya uaminifu? kuyashika maneno ya mtu husika,
ahadi, na majitoleo, bila kujali unapata ugumu au hatari ya namna gani.
Uaminifu ni sifa ya msingi ya Mungu na ndiyo anayoitegemea kutoka kwetu. Bahati
nzuri Mungu pia anatoa neema na nguvu ya kutusaidia kubaki waaminifu na
anatarajia sisi tuvitumie vema vipaji na neema atukirimiazo sisi. Wale wote
wanaojua mwalimu wao anahitaji nini (kama wafuasi wake) lakini wanatenda mambo
mabaya atakapo rudi atawaadhibu vibaya sana. Wale wote wasio jua (wasio
wafuasi, watu wa nje) bado wataadhibiwa kwa kufanya makosa lakini adhabu yao
itakuwa ndogo. Basi tusijifanye kuwa wajinga na kuziacha kazi na majukumu yetu.
Imani katika kipimo cha ukamilifu hutufanya sisi kuwa ‘waaminifu’ na wakati
tukiwa waaminifu, watu wanapata matumaini ‘kujiaminisha kwetu na kwa pamoja
tunajiunga na kumwamini Mungu na kuwa mwaminifu kwake. Je, sisi tu waaminifu
kwa Mungu na tupo tayari kumtolea yeye hesabu ya uaminifu wetu?
Sala: Tusaidie daima Bwana tuweze kuwa waaminifu, kwasababu kwa uaminifu
wetu ndiko tunako pata nguvu. Nisaidie mimi niweze kukutafuta daima na kuwa
tayari kila wakati kwa kujiandaa kwa ujio wako. Yesu nakuamini wewe. Amina
No comments:
Post a Comment