MASOMO YA MISA OKTOBA
27, 2023
IJUMAA, JUMA LA 29 LA
MWAKA
SOMO 1
Rum. 7:18-25
Najua ya kuwa ndani
yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema; kwa kuwa kutaka nataka,
bali kutenda lililo jema sipati. Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi;
bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo. Basi kama lile nisilolipenda ndilo
nilitendalo, si mimi nafsi yangu nilitendaye, bali ni ile dhambi ikaayo ndani
yangu.
Basi, nimeona sheria
hii, ya kuwa kwangu mimi nitakaye kutenda lililo jema, lipo lililo baya. Kwa
maana naifurahia sheria ya Mungu kwa utu wa ndani; lakini katika viungo vyangu
naona sheria iliyo mbali, inapiga vita na ile sheria ya akili zangu, na
kunifanya mateka ya ile sheria ya dhambi iliyo katika viungo vyangu.
Ole wangu, maskini mimi!
Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti? Namshukuru Mungu, kwa Yesu Kristo
Bwana wetu.
Neno la Bwana…
Tumshukuru Mungu.
_____________
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 119:66,76-77,93-94
(K) 68
(K) Unifundishe akili na
maarifa, Ee Bwana.
Unifundishe akili na
maarifa,
Maana nimeyaamini
maagizo yako.
Weew U mwema na mtenda
mema,
Unifundishe amri zako.
(K)
Nakuomba, fadhili zako
ziwe faraja kwangu,
Sawasawa na ahadi yako
kwa mtumishi wako.
Rehema sheria yako ni
furaha yangu. (K)
Hata milele sitayasahau
maagizo yako,
Maana kwa hayo
umenihuisha.
Mimi ni wako, uniokoe,
Kwa maana nimejifunza
mausia yako. (K)
_____________
SHANGILIO
2 Kor. 5:19
Aleluya, aleluya,
Mungu alikuwa ndani ya
Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, ametia ndani yetu neno la
upatanisho.
Aleluya.
_____________
INJILI
Lk. 12:54-59
Yesu aliwaambia makutano
pia, kila mwonapo wingu likizuka pande za magharibi mara husema, Mvua inakuja;
ikawa hivyo. Na kila ivumapo kaskazi, husema, Kutakuwa na joto; na ndivyo
ilivyo. Enyi wanafiki, mwajua kuutambua uso wan chi na mbingu; imekuwaje, basi,
kuwa hamjui kutambua majira haya?
Na mbona ninyi wenyewe
kwa nafsi zenu hamwamui yaliyo haki? Maana, unapofuatana na mshitaki wako
kwenda kwa mwamuzi, hapo njiani fanya bidi kupatanishwa naye, asije akakuburuta
mpaka mbele ya kadhi; yule kadhi akakutia mikononi mwake mwenye kulipiza, na
yule mwenye kulipiza akakutupa gerezani. Nakuambia, Hutoki humo kamwe hata
uishe kulipa senti ya mwisho.
Neno la Bwana… Sifa
kwako Ee Kristu.
_____________
Copyright © 2023,
"MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora –
Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see
www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment