“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Ijumaa, Oktoba 27, 2023
Juma la 29 la Mwaka
Rom 7: 18-25;
Zab 119: 66, 76-77, 93-94 (K) 68;
Lk 12: 54-59.
KUFAFANUA NYAKATI ZETU
Leo katika Injili ya Luka inafafanua ni kwa jinsi gani baadhi ya watu
walikuwa na uwezo wakusoma majira kwa mfano mawingu na mvua kipindi cha Yesu,
lakini wakashindwa kufafanua kipindi cha
Yesu ambacho Yesu mwenyewe alikiweka mbele ya macho yao kwa kuhubiri Neno la
Ufalme wa Mungu. Je, si kweli kwa
nyakati zetu pia?
Sisi tumebobea sana katika teknologia ya sayanzi na tunajivunia sana hali
hii. Lakini mara nyingi tunakosa ujumbe ambao Mungu anataka kutuambia. “alama za nyakati” ulikuwa ni ujumbe muhimu sana
wakati wa mkutano wa Vatican II ukituita kufafanua Neno la Mungu kulingana na
nyakati zetu bila kuharibu ujumbe wa
Yesu na mtazamo wa kanisa la kwanza na ujumbe wa Mababa wa kanisa. Kufafanua
wakati wetu maana yake kujikabidhi wenyewe kwenye ukweli. Tunapaswa kumtafuta
Yesu kwa moyo wote na kutaka yale yote ambayo yapo kwa ajili yake na kuacha
yale yasio ya kwakweli.
Jamii yetu inatuwekea maadili mbali mbali, tunaweza kujikuta sisi tukivutwa
huku na huku. Tunaweza kukuta kwamba akili zetu zimechukuliwa na tukakuta hata
kile muhimu cha ubinadamu wetu kimeharibiwa. Mfano sheria za kutoa mimba,
kuwaua watu kwa sindano eti kisa anateseka mno! Ndoa za kijadi! Maadili yetu yamevamiwa katika kila nyanja.
Kusoma alama za nyakati ni kuwa makini na kuyaona yote jinsi ulimwengu unavyo
jichanganya kila wakati na kulinda ukweli. Huku tukiona makosa yanayoletwa
kwenye maadili na tamaduni zetu.
Tafakari leo kama upo tayari kumkaribisha Roho wa ukweli akuongoze katika
kweli. Kuutafuta ukweli na kubaki nao ndio njia pekee ya kulinda maadili yetu
na kukwepa madhara yanaoletwa na teknolojia.
Sala:Bwana, nisaidie niweze kusoma alama za nyakati na kuona makosa yote
yanayo tokana nayo na pia uzuri wako unaoneakana katika hilo. nipe ujasiri na
nguvu niweze kukwepa kile kilicho kiovu
na kutafuta kile ambacho kinatoka kwako. Yesu nakuamini wewe. Amina.
No comments:
Post a Comment