MASOMO YA MISA OKTOBA
24, 2023
JUMANNE, JUMA LA 29 LA
MWAKA
SOMO 1
Rum. 5:12, 15, 17-21
Kwa mtu mmoja dhambi
iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu
wote kwa sababu wote wamefanya dhambi.
Kwa maana ikiwa kwa
kukosa kwake yule mmoja wengi walikufa, zaidi sana neema ya Mungu, na kipawa
kilicho katika neema yake mwanadamu mmoja Yesu Kristo kimezidi kwa ajili ya
wale wengi. Kwa maana ikiwa kwa kukosa mtu mmoja mauti ilitawala kwa sababu ya
yule mmoja, zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema, na kile kipawa cha haki,
watatawala katika uzima kwa yule mmoja, Yesu Kristo. Basi tena, kama kwa kosa
moja watu wote walihukumiwa adhabu, kadhalika kwa tendo moja la haki watu wote
walihesabiwa haki yenye uzima. Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu
wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa kutii kwake mmoja
watu wengi wameingizwa katika hali ya wenye haki. Lakini sheria iliingia ili
kosa lile liwe kubwa sana; na dhambi ilipozidi, neema ilikuwa nyingi zaidi; ili
kwamba, kama vile dhambi ilivyotawala katika mauti, vivyo hivyo kwa njia ya
haki neema itawale hata uzima wa milele kwa Yesu Kristo Bwana wetu.
Neno la Bwana…
Tumshukuru Mungu.
_____________
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 40:6-9, 17 (K) 8, 9
(K) Tazama nimekuja, Ee
Bwana, kuyafanya mapenzi yako.
Dhabihu na matoleo
hukupendezwa nazo,
Masikio yangu
umeyazibua,
Kafara na sadaka za
dhambi hukuzitaka.
Ndipo niliposema, Tazama
nimekuja. (K)
Katika gombo la chuo
nimeandikiwa;
Kuyafanya mapenzi yako,
Ee Mungu wangu, ndiyo
furaha yangu;
Naam, sheria yako imo
moyoni mwangu. (K)
Nimehubiri habari za
haki katika kusanyiko kubwa,
Sikuizuia midomo yangu;
Ee Bwana, unajua. (K)
Nami ni maskini na
mhitaji,
Bwana atanitunza.
Ndiwe msaada wangu na
mwokozi wangu,
Ee Mungu wangu,
usikawie. (K)
_____________
SHANGILIO
Yn. 10:27
Aleluya, aleluya,
Kondoo wangu waisikia
sauti yangu, nami nawajua, nao wanifuata.
Aleluya.
_____________
INJILI
Lk. 12:35-38
Yesu aliwaambia
wanafunzi wake: Viuno vyenu na viwe vimefungwa, na taa zenu ziwe zinawaka;
nanyi iweni kama watu wanaomngojea bwana wao, atakaporudi kutoka arusini, ili
atakapokuja na kubisha, wamfungulie mara. Heri watumwa wale, ambao bwana wao
ajapo atawakuta wanakesha. Amin, nawaambieni, atajifunga na kuwakaribisha
chakulani, atakuja na kuwahudumia. Na akija zamu ya pili, au akija zamu ya
tatu, na kuwakuta hivi, heri watumwa hao.
Neno la Bwana… Sifa
kwako Ee Kristo.
_____________
Copyright © 2023,
"MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora –
Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment