“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Jumanne, Oktoba 24, 2023,
Juma la 29 la Mwaka
Rom 5: 12, 15, 17-21;
Zab 40: 6-9, 17 (K) 8,9;
Lk 12: 35-38.
KUWA MWEPESI KUMKARIBISHA YESU
Yesu anagonga ndani ya moyo wako. Anakuja mara nyingi anatamani kuingia
ndani kukaa na wewe ili aweze kuongea na wewe, kukupatia nguvu na kukuponya na
kukusaidia. Swali la kweli la kujiuliza je, ni kwa kiasi ghani upo tayari
kumpokea mara moja? Mara nyingi tunaona shaka kumpokea Kristo. Mara nyingi
tunataka kwanza tufahamu mpango wetu kwanza kabla hatuja jikabidhi kwa Yesu.
Tunachopaswa kufahamu ni kwamba Yesu ni mwaminifu kwa kila Nyanja. Ana jibu
la kila swali ambalo tunaweza kuwa nalo katika maisha yetu. Je, unaamini hili?
Je, unakubali ukweli huu? Kama tutakubaliana na hili tutakuwa tayari kufungua
mioyo yetu na kumpokea bila kusitasita na kupokea neema yake. Tutakuwa makini
kweli kweli kwa kile ambacho Yesu anataka kutuambia sisi na neema ambayo anataka
kutupatia.
Tafakari leo, upo tayari kiasi ghani kufungua mara moja kila aina ya
ufahamu wa maisha yako kwa ajili ya neema na mapenzi ya Mungu. Mkaribishe ndani
kwa furaha na shauku kuu na ruhusu mpango wake uendelee kujifunua katika maisha
yako.
Sala: Bwana, ninatamani kukuweka wewe katika moyo wangu utembee katika
maisha yangu uzame ndani kila siku. Ninatamani kusikia sauti yako na kujibu kwa
moyo wote. Nipe neema niweze kuitika vyema kama inavyo stahili. Yesu, nakuamini
wewe. Amina..
No comments:
Post a Comment