MASOMO YA MISA, OKTOBA
22, 2023
DOMINIKA YA 29 MWAKA A
MWANZO:
Zab. 17:6,8
Ee Mungu, nimekuita kwa
maana utaitika, utege sikio lako ulisikie neno langu. Ee Bwana, unilinde kama
mboni ya jicho, unifiche chini ya uvuli wa mbawa zako.
________
SOMO 1
Isa. 45:1, 4-6
Haya ndiyo Bwana
amwambiayo Koreshi, masihi wake, ambaye nimemshika mkono wake wa kuume, ili
kutiisha mataifa mbele yake, nami nitalegeza viuno vya wafalme, ili kufungua
milango mbele yake, hata malango hayatafungwa. Kwa ajili ya Yakobo, mtumishi
wangu, na Israeli, mteule wangu, nimekuita kwa jina lako; nimekupa jina la
sifa; ijapokuwa hukunijua. Mimi ni Bwana, wala hapana mwingine; zaidi yangu
mimi hapana Mungu; nitakufunga mshipi ijapokuwa hukunijua; ili wapate kujua
toka maawio ya jua, na toka magharibi, ya kuwa hapana mwingine zaidi ya mimi.
Neno la Bwana…
Tumshukuru Mungu.
________
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 96:1, 3-5, 7-10 (K)
7
(K) Mpeni Bwana utukufu
na nguvu.
Mwimbieni Bwana wimbo
mpya, Mwimbieni Bwana, nchi yote.
Wahubirini mataifa
habari za utukufu wake,
Na watu wote habari za
maajabu yake. (K)
Kwa kuwa Bwana ni mkuu
mwenye kusifiwa sana,
Na wa kuhofiwa kuliko
miungu yote.
Maana miungu yote ya
watu si kitu,
Lakini Bwana ndiye
aliyezifanya mbingu. (K)
Mpeni Bwana enyi jamaa
za watu,
Mpeni Bwana utukufu na
nguvu.
Mpeni Bwana utukufu wa
jina lake.
Leteni sadaka mkaziingie
nyua zake. (K)
Mwabuduni Bwana kwa
uzuri wa utakatifu,
Tetemekeni mbele zake,
nchi yote.
Semeni katika mataifa,
Mungu ni mfalme,
Atawahukumu watu kwa
adili. (K)
________
SOMO 2
1Thes. 1:1-5
Paulo, na Silwano, na
Timotheo, kwa kanisa la Wathesalonike, lililo katika Mungu Baba, na katika
Bwana Yesu Kristo. Neema na iwe kwenu na amani.
Twamshukuru Mungu
sikuzote kwa ajili yenu nyote, tukiwataja katika maombi yetu. Wala hatukuachi
kuikumbuka kazi yenu ya imani, na taabu yenu ya upendo, na saburi yenu ya
tumaini lililo katika Bwana wetu Yesu Kritu, mbele za Mungu Baba yetu. Kwa
maana, ndugu mnaopendwa na Mungu, twajua uteule wenu; ya kwamba injili yetu
haikuwafikia katika maneno tu, bali na katika nguvu, na katika Roho Mtakatifu,
na uthibitifu mwingi.
________
SHANGILIO
Yn. 15:15
Aleluya, aleluya,
Ninyi nimewaita rafiki,
kwa kuwa yote niliyoyasikia, kwa Baba yangu nimewaarifu.
Aleluya.
________
INJILI
Mt. 22:15-21
Mafarisayo walienda zao,
wakafanya shauri, jinsi ya kumtega Yesu kwa maneno. Wakatuma kwake wanafunzi
wao pamoja na Maherodi, wakasema, Mwalimu, twajua ya kuwa wewe u mtu wa kweli,
na njia ya Mungu waifundisha katika kweli, wala hujali cheo cha mtu awaye yote,
kwa maana hutazami sura za watu. Basi utuambie, Waonaje? Ni halali kumpa
Kaisari kodi, ama sivyo? Lakini Yesu akaufahamu uovu wao, akasema, Mbona
mnanijaribu, enyi wanafiki? Nionyesheni fedha na kodi. Nao wakamletea dinari.
Akawaambia, Ni ya nani sanamu hii, na anwani hii? Wakamwambia, Ni ya Kaisari.
Akawaambia, Basi, mlipeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na Mungu yaliyo ya Mungu.
Neno la Bwana… Sifa
kwako Ee Krist0.
________
Copyright © 2023,
"MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora –
Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see
www.fur-kat.blogspot.com.
Mungu ni mwema
ReplyDeleteMwenyezi Mungu anatenda hakika tumuombe bila kuchoka nasi tutabalikiwa Kwa kadri ya fadhiri zetu
ReplyDelete