“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Jumanne, Oktoba 14, 2025,
Juma la 28 la Mwaka
Rom 1: 16-25;
Zab 19: 2-5 (K) 2;
Lk 11: 37-41.
KUONDOA UNAFIKI WOTE!
Mafarisayo walijivuna wenyewe kuwa wema na wasafi kwa kushika sheria na
mapokeo. Waliigawa jamii katika makundi mawili, walio wema na walio waovu,
wakijiona wao kuwa watu wema na watu wa Mataifa kuwa waovu. Kwa njia ya sheria
zao walizo jitengenezea walifunga ufalme wa Mungu kwa mataifa mengine, na
walioneka kuwa waovu kwao. Walijitahidi kuonekana wema machoni pa watu lakini
mioyo yao ilikuwa imejaa unafiki na uovu. Majivuno yao yaliwafanya wahangaike
na kuhangaikia vitu vya nje, ili waoneakane wenye haki. Mbaya zaidi muonekano
wao wa njee ulikuwa ni kama mtu aliye jifunika kwa gamba la wema lakini ndani
kuna uovu. Yesu anawaita “wapumbavu”.
Hata sisi twaweza kuwa kama wao mara nyingine. Sisi tunaweza kuhangaika
sana kuhusu muonekano wetu wa njee, lakini ndani tupo mbali kabisa na Mungu.
Lakini kipi kilicho cha muhimu zaidi? Kilicho cha muhimu ni kile ambacho Mungu
anaona ndani mwetu? Mungu anaona ndani na kila lengo tulilo nalo. Anaona nia
zetu, fadhila zetu, dhambi zetu, tulipo jishikilia na yote yaliofichika machoni
pa wengine. Sisi wote tunaitwa kuona kile ambacho Yesu anakiona. Tunaitwa
kuangalia mioyo yetu kwenye mwanga wa ukweli.
Tafakari leo juu ya roho yako. Usiogope kuiangalia katika mwanga wa ukweli
na kuyaona maisha yako kama Mungu anavyo yaona. Hii ndio hali ya kwanza kabisa
ya kutaka kupata utakatifu. Sio njia tu ya kusafisha mioyo yetu, ni nafasi ya
kuruhusu muonekano wetu wa njee kungara kwa mwanga wa kweli wa Mungu kutoka
ndani.
Sala: Bwana, ninataka kuwa Mtakatifu. Ninataka kujiosha tena na tena.
Ninaomba nione moyo wangu kama unavyo uona na kuruhusu neema na huruma
vinitakase mimi katika njia ambayo unataka kunitakasa. Yesu, ninakuamini wewe.
Amina.

No comments:
Post a Comment