“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya Kila siku
Jumanne, Oktoba 3, 2023
Juma la 26 la Mwaka
Zek 8: 20-23;
Zab 86: 1-7;
Lk 9: 51-56
KUKABILIANA NA KUKATALIWA!
Injili ya Luka leo, inanikumbusha kwamba, kwasababu tu watu hawaendani au
hawakidhi viwango vyangu haimanishi tupaswa kuwahukumu. Mungu ametuumba sisi
wote kama kiumbe pekee tulio na kazi ya kutimiza katika maisha. Pengine watu wa
kijiji cha Samaria hawakuwa watu waliojali ujio wa Yesu, lakini kijiji kingine
walichukua nafasi yao na kumjali. Hatupaswi kukata tamaa wakati maisha yanavyo
“enda kinyume na mapenzi yetu”- bali tunapaswa kubaki katika uhusiano na Mungu
kila mara, na kuamini kwamba kila tukio linatokea kwa lengo fulani. Tunapaswa
kuwa watu wa sala na matumaini tusio na hofu na badala yake kuamini kwamba
Mungu atatuongoza kwenye malengo yetu.
Yakobo na Yohane, walitaka mji wa Samaria ulaaniwe kwasababu
haukumkaribisha Yesu, kwani walikuwa wameumizwa na kukataliwa. Kukataliwa na
aina nyingine zinazo sababishwa na wengine zinaweza kuwa vigumu kuziachia
ziondoke. Zinaweza kukaa ndani ya mioyo yetu na baadae kukuwa na kuchukuwa
nafasi. Tukiwa na hali ya namna hii tutapata wakati mgumu sana wa kusamehe na
kuachia mambo yatoke. Njia nzuri ya kuachia mambo yatoke ndani ya mioyo yetu ni
kufanya kama Yesu alivyo fanya. Tunapaswa kuachia na kuendelea mbele. Mungu
mwenyewe ndiye mwenye kulipiza sio kazi yetu. Tunavyo shindwa kufanya hili,
maumivu yana tuumiza sisi zaidi kuliko mtu mwingine.
Tafakari leo juu ya kinyongo ulicho shikilia bado katika moyo wako
kwasababu ya kuumizwa na mtu Fulani. Fanya uamuzi sahihi wa kusamehe na kusonga
mbele. Kusamehe sio kujifanya kama vile kitendo ulicho tendewa hukufanyiwa wewe
au basi tu. Bali, kitendo cha kumsamehe mwenzako ni hali ya kuonesha kuwa
kulikuwa na kosa. Msamaha unakuruhusu wewe na kukupatia wewe nafasi ya kukuwa
na kuachana na maumivu ambayo yangekupata kwasababu ya tendo ulilo fanyiwa.
Lakini mwishoni linafungua mlango kwa aliyekosa kuweza kutubu na kutafuta
msamaha nawe. Acha kisasi na lawama atoe Mungu na tafuta kuweka moyo wako
katika Amani.
Sala: Bwana, nina sali kwa ajili ya neema ya msamaha. Nina wasamehe wote
walio niumiza mimi zaidi na nina wakabidhi kwako. Nawasamehe. Ninakupenda wewe
Bwana wangu. Nisaidie mimi niwapende wengine kama wewe unavyo wapenda. Yesu,
ninakuamini wewe. Amina
Copyright ©2013-2023 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see
www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment