“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya Kila siku
Jumatano, Oktoba 4, 2023
Juma la 26 la Mwaka
Kumbukumbu ya Mt. Fransisko wa Assis
Neh 2: 1-8;
Zab 136: 1-6;
Lk 9: 57-62
GHARAMA YA KUWA MFUASI WA KRISTO!
Tunaishi katika ulimwengu ambao gharama za maisha zinapanda kadiri ya
mahitaji yanavyopanda. Na wakati mwingine kadiri gharama inavyopanda ndivyo
tunavyo hitaji zaidi. Kuna gharama ya kumfuata Kristo pia! Katika Injili, watu
watatu wanakuja kwa Yesu na wanataka kumfuata. Lakini Yesu alivyo ongea kuhusu
gharama ya kumfuata hawakuwa tayari kuilipa. Walitaka kuwa na Yesu lakini
katika hali yao wenyewe. Hawakuwa tayari kuachia mambo yao, tamaa zao, mipango
yao n.k, kwa ajili ya Kristo.
Haishangazi kwani hata Yesu alisema njia ya kwenda kwenye uzima wa milele
ni nyembamba na ni wachache watakao ipata. Nehemia alikuwa mbeba kikombe katika
mahakama ya Mfalme Artaxerxes. Mbeba kikombe alikuwa ni mtu mwenye madaraka
makubwa katika mahakama, ambaye kazi yake kubwa ilikuwa pia kuhudumia vinywaji
katika meza ya kifalme. Mtu mwenye hofu na mabaya, na mwenye kuhesabiwa adabu
njema ndiye pekee aliyeweza kupewa mamlaka haya. Alikuwa na kazi ya kulinda
kikombe cha mfalme asije akawekewa sumu, na alikuwa lazima anywe divai kidogo
mbele ya watu kabla haja anza kuhudumia watu. Nehemia, ambaye ni mgeni katika
nchi ya kigeni, alionekana mtu mwenye kuaminika. Kwa kutambua kwamba kuta za
Yerusalem zilikuwa zimebomoka alimwuomba ruhusa Mfalme aende kuzijenga.
Artaxerxes alimtuma kama gavana wa Yuda ili aende kuzijenga kuta hizo. Akiwa
huko, aliwapa changamoto kwa kuwapinga maadui wa Yuda pande zote-Wasamaria,
Waamori, Waarabu na Wafilisti na akajenga kuta hizo kwa muda wa siku 52.
Kinacho tugusa sisi ni upendo wa Nehemia kwa mji wa Yerusalem, mji Mtakatifu,
ambao pia ulikuwa na hekalu-nyumba ya Mungu. Je, ni upendo gani tulionao juu ya
nyumba ya Mungu na utume wa Bwana? Je, tumejitoa kiasi ambacho tunaweza kuweka
maisha yetu katika hatari?
Wito wa Yesu. Anapo tuita sisi tunapaswa kuitika kwa moyo wote na kujitoa
kabisa kwa moyo wetu wote na kwa ukarimu wote. Katika somo la Injili, Bwana
alitamani yule mtu wa tatu mara moja angemfuata mara moja. Lakini huyu mtu
anageuka nyuma anataka aende kwanza kwenda kuwaaga kwanza nyumbani. Lakini Yesu
anaweka wazi kwamba yeyote yule anayeitwa anapaswa kuitika mara moja na
kumfuata. Yesu anatumia wakati huu kutukumbusha kwamba utume wetu wa kwanza ni
kuitika na kwenda kufanya kazi yake. Katika wito wetu wa kumfuata Kristo,
tunapaswa kuwa tayari kumfuata Kristo, tunapaswa tuitike bila kuangalia angalia
nyuma. Katika maisha yetu wenyewe, tunaweza tusipate ule wito wa kuacha kila
kitu katika hali ya kuacha vyote na kuondoka kumtumikia Kristo katika hali
nyingine ya maisha. Lakini hapa cha muhimu ni utayari wetu na majitoleo yetu
juu ya nyumba ya Mungu.
Katika siku hii tunapo mkumbuka Mt. Fransisko wa Assis yeye alimfuata Yesu
bila kujibakiza kwa kuacha mali na anasa mbali mbali na hivyo kumfuata Kristo
mwenyewe katika hali ya ukaribu kabisa. Yeye aliipenda nyumba ya Mungu, ambayo
katika maono aliambiwa akaijenge kwani inabomoka. Kwa maisha yake aliwavuta
wengi mno kwa Kristo na ndio maana hata siku hizi yapo mashirika mengi sana
yanayo fuata karama yake. Tuwaombee Wafransisko wote waendelee kumtangaza Kristo
kwa maisha yao.
Sala: Bwana, ninakupenda wewe na ninataka kukufuata wewe. Nisaidie mimi
niweze kushinda kitu chochote kinacho weza kunirudisha nyuma nishindwe kusema
“ndiyo” kwa wito wa kutimiza mapenzi yako matakatifu. Yesu nakuamini wewe.
Amina.
Copyright ©2013-2023 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see
www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment