“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Jumamosi, Septemba 30, 2023
Juma la 25 la Mwaka
Kumbukumbu ya Mt. Jerome, Mwalimu wa Kanisa
Zek 2: 5-9, 14-15;
Yer 31: 10-12, 13;
Lk 9: 43-45
ROHO MTAKATIFU ANAFUMBUA MAFUMBO YA IMANI!
Yesu katika Injili anongea kuhusu kifo chake. Lakini wanafunzi wake
hawaelewi mafumbo haya makuu. “Walishindwa kufahamu ana maanisha nini lakini
wakaogopa kumuuliza nini maana ya msemo huo” . Lakini Yesu hakuumizwa na hali
yao ya kutokuelewa. Alifahamu kwamba hawata elewa mara moja. Lakini hili
halikumzuia kuacha kuwaambia. Kwasababu alitambua muda utafika tuu watakuja
kuelewa tu. Wataelewa haya wakati Roho Mtakatifu atakapo washukia na kuwaambia
kweli yote. Hii ni kazi ya Roho Mtakatifu ili kuelewa haya mafumbo makuu.
Ni kweli pia kwa upande wetu. Tunapokumbana na mafumbo haya ya mateso ya
Yesu, na wakati tunapo kumbana na mateso yetu wenyewe au mateso ya wale tunao
wapenda, tunaweza tuka changanyikiwa kwanza. Tunahitaji zawadi ya Roho
Mtakatifu ili tuweze kuelewa mafumbo haya. Mateso hayakwepeki. Sisi wote
tunavumilia mateso. Na kama hatutamrushusu Roho Mtakatifu atembee katika maisha
yetu tutaishi katika kuchanganyikiwa na kuwa na mashaka daima. Lakini kama
tukimruhusu Roho Mtakatifu afungue akili zetu, tutaanza kuelewa ni kwa jinsi
gani Mungu anafanya katika katika maisha yetu katika mateso yetu, kama alivyo
leta ukombozi ulimwenguni kwa njia ya mateso, kifo na ufufuko wa Kristo.
Je, unataka Roho Mtakatifu akufunulie maana na thamani ya mateso katika
maisha yako? Sali kwa Roho Mtakatifu ukimuomba neema na umwache Mungu akuongoze
katika chemchemi ya mafumbo haya ya Imani.
Leo, tunasherekea kumbukumbu ya Mt. Jerome, ambaye anajulikana kama Baba wa
elimu ya sayanzi ya Biblia, ni yeye aliye tafsiri Agano la Kale la Kiebrania na
Agano Jipya la Kigiriki kwenda katika lugha ya Kilatini. Alisema kwamba;
“ujinga wa kutokufahamu maandiko, ni ujinga wa kutokumfahamu Kristo”.
Sala: Bwana, ninatambua kuwa uliteseka na ukafa kwa ajili ya wokovu wangu.
Ninatambua mateso yangu yanaweza kuleta maana mpya katika msalaba wako.
Nisaidie niweze kufahamu mafumbo haya makuu niweze kufahamu thamani kubwa
katika msalaba wako na wangu pia. Yesu, ninakuamini wewe. Amina
Copyright ©2013-2017 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment