
MASOMO YA MISA, JUMATATU, SEPTEMBA 8, 2025
JUMA LA 23 LA MWAKA
SIKUKUU YA KUZALIWA BIKIRA MARIA MTAKATIFU
SOMO 1
Rum. 8:28 – 30
Twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya
kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa
kusudi lake. Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili
wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni
mwa ndugu wengi. Na wale aliowachagua tangu asili, hao akawaita; na wale
aliowaita, hao akawahesabia haki; na wale aliowahesabia haki, hao akawatukuza.
Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.
________
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 13:5 – 6 (K) Isa. 61:10
(K) Nitafurahi sana katika Bwana.
Nami nimezitumainia fadhili zako;
Moyo wangu na uufurahie wokovu wako. (K)
Naam, nimwimbie Bwana,
Kwa kuwa amenitendea kwa ukarimu. (K)
________
INJILI
Mt. 1:1 – 16, 18 – 23
Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo, mwana wa Daudi,
mwana wa Ibrahimu.
Ibrahimu alimza Isaka; Isaka akamzaa Yakobo;
Yakobo akamzaa Yuda na ndugu zake; Yuda akamzaa Peresi na zera kwa Tamari;
Peresi akamzaa Esromu; Esromu akamzaa Aramu; Aramu akamzaa Aminadabu; Aminadabu
akamzaa Nashoni; Nashoni akamzaa Salmoni; Salmoni akamzaa Boazi kwa Rahabu;
Boazi akamzaa Obedi kwa Ruthu; Obedi akamzaa Yese; Yese akamzaa mfalme Daui.
Daudi akamzaa Sulemani kwa yule mke wa Uria; Sulemani akamzaa Rehoboamu;
Rehoboamu akamzaa Abiya; Abiya akamzaa Asa; Asa akamzaa Yehoshafati;
Yehosahafati akamzaa Yoramu; Yoramu akamzaa Uzia; Uzia akamzaa Yothamu; Yothamu
akamzaa Ahazi; Ahazi akamzaa Hezekia; Hezekia akamaza Yosia; Yosia akamzaa
Yekonia na ndugu zake, wakati wa ule uhamisho wa Babeli. Na baada ya ule
uhamisho wa Babeli, Yekonia akamzaa Shealtieli; Shealtieli akamzaa Zerubabeli;
Zerubabeli akamzaa Abihudi; Abihudi akamzaa Eliakimu; Eliakimu akamzaa Azori;
Azori akamzaa Sadoki; Sadoki akamzaa Akimu; Akimu akamzaa Eliudi; Eliudi akamzaa
Eleazari; Eleazari akamzaa Matani; Matani akamzaa Yakobo; Yakobo akamzaa Yusufu
mumewe Mariamu aliyemzaa Yesu aitwaye Kristo.
Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi.
Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu
kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu. Naye
Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu
kumwacha kwa siri. Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana
alimtoke katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa DAudi, usihofu kumchukua
Mariamu mkeo, maana mbimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu. Naye atazaa
mwana, nawe utwamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake
na dhambi zao. Hayo yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa
ujumbe wa nabii akisema, Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao
watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi.
Neno la Bwana...Sifa kwako, ee Kristo
________
Copyright © 2025, "MASOMO YA MISA"
published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings reproduced by
Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment