MASOMO YA MISA, JUMATATU, SEPTEMBA 15,
2025
JUMA LA 24 LA MWAKA
KUMBUKUMBU YA BIKIRA
MARIA MTAKATIFU WA MATESO
SOMO 1
Ebr. 5:7 – 9
Kristo, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule,
awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na
machozi, akasikilizwa wa jinsi alivyokuwa mcha Mungu; na, ingawa ni Mwana,
alijifunza kutii kwa mates ohayo yaliyompata; naye alipokwisha kukamilishwa,
akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii.
Neno la Bwana…
Tumshukuru Mungu.
________
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 31:1 – 5, 14 – 15,
19 (K) 16
(K) Uniokoe, Ee Bwana,
kwa ajili ya fadhili yako.
Nimekukimbilia Wewe, Bwana,
Nisiaibike mbele kwa haki yako uniponye.
Unitegee sikio lako, uniokoe hima. (K)
Uwe kwangu mwamba wa nguvu,
Nyumba yenye maboma ya kuniokoa,
Ndiwe genge langu na ngome yangu,
Kwa ajili ya jina lako uniongoze, unichunge. (K)
Utanitoa katika wavu walionitegea kwa siri,
Maana wewe ndiwe ngome yangu.
Mikononi mwako naiweka roho yangu,
Umenikomboa, Ee Bwana, Mungu wa kweli. (K)
Lakini mimi nakutumaini Wewe, Bwana,
Nimesema, Wewe ndiwe Mungu wangu.
Nyakati zangu zimo mikononi mwako;
Uniponye na adui zangu, nao wanaonifuatia. (K)
Jinsi zilivyo nyingi fadhili zako
Ulizowawekea wakuchao;
Ulizowatendea wakukimbiliao
Mbele ya wanadamu! (K)
________
SHANGILIO
Aleluya, aleluya,
Bikira Maria anafurahi yeye ameshinda na kupata
nishani ya ushahidi pasipo kufa, alipokuwa chini ya msalaba wa Bwana.
Aleluya.
________
INJILI
Yn. 19:25 – 27
Penye msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama
mamaye, na umbu la mamaye, Mariamu wa Klopa, na Mariamu Magdalene. Basi Yesu
alipomwona mama yake, na yule mwanafunzi aliyempenda amesimama karibu,
alimwambia mama yake, Mama, tazama, mwanao. Kisha akamwambia yule mwanafunzi,
Tazama, mama yako. Na tangu saa ile mwanafunzi yule akamchukua nyumbani mwake.
Neno la Bwana… Sifa
kwako Ee Kristo.
Au
INJILI
Lk. 2:33 – 35
Babaye na mamaye wa Yesu walikuwa
wakiyastaajabia hayo yaliyonenwa juu yake. Simeoni akawabariki, akamwambia
Mariamu mama yake, Tazama, huyu amewekwa kwa kuanguka na kuinuka wengi walio
katika Israeli, na kuwa ishara itakayonenewa. Nawe mwenyewe, upanga ukaingia
moyoni mwako, ili yafunuliwe mawazo ya mioyo mingi.
Neno la Bwana… Sifa
kwako Ee Kristo.
________
Copyright © 2025, "MASOMO YA MISA"
published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings reproduced by
Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment