“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Jumatano, Septemba 27, 2023
Juma la 25 la Mwaka
Kumbukumbu ya Mt. Vinsenti wa Paulo
Ezra: 9: 5-9;
Tob 13: 2,4,6-8;
Lk 9: 1-6
KUNGUTA MAVUMBI: NAKUACHA MAMBO YA ZAMANI
Yesu alikuwa amemaliza kuwaambia wafuasi wake juu ya kwenda mji baada ya
mji ili kuhubiri Injili/ aliwaambia wasichukue chakula wala nguo ya ziada
njiani, bali wategemee ukarimu wa wale ambao wanaenda kuwahubiria. Mwandishi wa
Methali anasali “Bwana usinifanye mimi tajiri wala usinifanye maskini” (Methali
30:8), kwasababu tukiwa tajiri sana tunaweza kumsahau Mungu, na hata tukiwa
maskini sana, tunaweza kuiba na hivyo kujikuta tunaenda mbali na Mungu.
Ana waambia pia watu wengine hawata wapokea. Aliwaambia wakungute mavumbi
ya miguu yao wanapo ondoka katika mji huo. Hili lina maana ya vitu viwili. Cha
kwanza, tunapo kataliwa tunaweza kuumia sisi wenyewe, ni rahisi kukaa na kuumia
na kuwa na hasiri na matokeo yake kuruhusu kukataliwa kwetu kukaleta madhara zaidi
kwetu. Pili, ni njia ya kusema kwamba tunapaswa kusonga mbele daima. Hatupaswi
kukaa chini na kuanza kuwaza kwanini wametukataa, bali tunapaswa kusonga mbele
na kuendela kuwatafuta wale walio tayari kupokea ujumbe wa Yesu, yaani Injili.
Kukunguta mavumbi maana yake ni sehemu ya kusema kwamba siruhusu kukataliwa
kwangu kuniumize na kushindwa kwenda mbele. Ni njia ya kusonga mbele na
kujiambia kwamba siruhusu niongozwe na mawazo mabaya ya wengine. Ujumbe huu wa
Yesu sio kwamba unalenga wale wanao tukataa, bali ni kwanza kabisa kuwatafuta
wale ambao watatupokea sisi na ujumbe wa Yesu wa Injili ambayo tunapaswa
kuitoa.
Tutafakari juu ya uchungu uliobeba moyoni daima kwasababu ya kukataliwa na
wengine. Mungu leo anatuita tuachie, tukungute mavumbi na kuanza kuwatafuta
wengine kwa mapendo ili tuweze kushiriki upendo wa Kristo na wao.
Sala: Bwana, ninapo kutana na kukataliwa na kuumia, ninaomba unisaidie
niondoe hasira ambayo naweza kuwa nayo. Nisaidie niweze kuendelea na utume
wangu wa mapendo na kuendelea kushirikisha Injili yako nao walio tayari
kuipokea. Yesu, nakuamini wewe. Amina
Copyright ©2013-2023 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see
www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment