“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Jumatano, Juni 21, 2023
Juma la 11 la Mwaka
Kumbukumbu Mt. Aloisi Gonzaga
2 Kor 9: 6-11;
Zab 112: 1-4, 9;
Mt 6:1-6, 16-18
UTAKATIFU WA KWELI!
Wayahudi walichukulia sala, kufunga na kutoa sadaka kama nguzo tatu ambapo
maisha mazuri yalijikita. Kwanini tunasali, kufunga na kutoa sadaka? Je,
nikutaka ujulikane na watu wakutazame kwamba wewe ni mtu wa juu na unajua
kusali na kufunga? Au ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu? Yesu anawaonya wafuasi
wake juu ya hili la kutafuta utukufu binafsi. Utakatifu wa kweli ni zaidi ya
kujisikia vizuri au kuonekana mtakatifu mbele ya watu. Ni hali ya heshima,
kujitoa, kusujudu, kuabudu na utii. Ni zawadi ya Roho Mtakatifu inayofanya kazi
ndani yetu ikitufanya tuelekeze maisha yetu kwa Mungu tukiwa na hali takakatifu
yakutaka kumpendeza Mungu katika vitu vyote. Tukifanya vyote kwa utukufu wake.
Wayahudi walijulikana kwa kujitoa kwao katika sala. Sala ya kawaida ilikuwa
na sehemu tatu kwa siku. Na Marabi walikuwa na sala maalumu kwa kila tukio.
Yesu anawaonya wafuasi wake juu ya sala kuonekana kama kitu cha kawaida,
kufanya sala kama mashine hivi, kuondoa maana halisi, na kuwa na wazo dogo la
Mungu ndani yake. Katika sala Yesu aliyotufundisha sisi, tunathubutu kumuita
Mungu ‘Baba yetu’ tukiomba mambo tunayohitaji sisi kama watoto wake. Ni kwa
njia ya Roho Mtakatifu tunaweza kumfahamu Mungu na kumuita ‘Abba, Baba’ (Rum 8:
15). Wakati tunamuita Mungu atusaidie wakati mwingine hatupi tunachotaka sisi
kwa wakati huo. Badala yake anajibu kwa neema na huruma. Yeye anatujalia na
anatusamehe na anatutaka na sisi tuwafanyie wengine hivyo hivyo kama anavyofanya
kwetu. Je, unawatendea wengine kama Mungu anvyopenda tuwatendee? Au unawatendea
wengine kama Mungu anavyowapa neema na rehema?
Sala: Bwana, nisaidie niweze kuishi maisha ya neema. Nisaidie niweze
kukutumikia wewe hata ikiwa hakuna anaye ona. Katika hali hii, tuletee neema na
huruma kwa ajili ya Ulimwengu. Yesu nakuamini wewe. Amina.kula cha malaika.
Yesu, nakuamini wewe. Amina.
No comments:
Post a Comment