“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Jumamosi, Juni 24, 2023
Juma la 11 la Mwaka wa Kanisa
Sherehe ya kuzaliwa kwa Mt.Yohane Mbatizaji
Is 49: 1-6;
Zab 138: 1-3, 13-15;
Mdo13: 22-26;
Lk 1: 57-66, 80
ISHARA YA UTUKUFU YA JUA LA HAKI !
Kwa kawaida Kanisa alisheherekei sikukuu za kuzaliwa za watakatifu. Lakini
kuna sikukuu nyingine za pekee ambazo ni kuzwaliwa Bwana wetu Yesu Kristo-na
sherehe za kuzaliwa Bikira Maria naya kuzawaliwa kwa Yohane mbatizaji. Hii ni
kwasababu Maria, tangu kuumbwa kwake kwanza alikingiwa dhambi ya asili. Yohane
Mbatizaji alitakaswa kutoka dhambi ya asili akiwa tumboni mwa mama yake. Leo
inajulikana kama “Noeli ndogo” kwasababu Yohane alimtangulia Yesu na alimbatiza
Kristo. Maisha ya Yohane Mbatizaji yalijazwa na jambo moja-kumuonesha Yesu kwa
watu na kuandaa ujio wa Ufalme wa Mungu. Maandiko matakatifu yanatuambia kwamba
Yohane Mbatizaji alijazwa na Roho Mtakatifu hata angali tumboni mwa mama yake
(Lk 1: 15, 41) na Kristo mwenyewe ambaye Bikira Maria alipata mimba kwa uwezo
wa Roho Mtakatifu. Moto wa Roho Mtakatifu ulimjaza Yohane na akawa mtangulizi
wa Masiha. Yohane alivunja ukimya wa manabii wa karne zilizopita alipoanza
kuongelea kuhusu Neno wa Mungu kwa watu wa Israeli. Akiwa katikati ya watu
waliopoteza matumaini yao kuhusu Mungu, sasa anaiamsha tena Imani yao,
kuwatahadharisha kuhusu usafi wa mioyo yao, kuamsha tena ndani yao mapenzi mema
ya kumtambua na kumkubali Masiha anayekuja. Watu walikimbilia jangwani kwenda
kumsikiliza na kubatizwa.
Yohane aliitwa kutoka tumboni mwa mama yake kuwa mjumbe wa ufalme wa Mungu.
Kwa njia hiyo hiyo Yesu naye anatualika sisi tuliowafuasi wake na tuliobatizwa
kwa jina lake, tuweze kuwa manabii- tuwe watu wanaotangaza kwa maneno na
matendo ujumbe wa haki na huruma. Tangu ubatizo wetu (Kuzaliwa katika maisha ya
Kimungu) sisi kama Yohane, tuna utume wakufanya kutoka katika mpango wa Baba
yetu. Sio tuu kumfuata Yesu, bali kutangaza siku ya ukombozi tunayo tumaini
ndani ya kristo kwamba itatimilizwa.
Tutafakari leo, hasa katika zile hali ambazo hatukuwa waaminifu kwa Mungu
katika maisha yetu. Mungu atatupokea tena na kubadilisha maisha yetu. Mungu
anatusubiri na huruma yake haina kikomo. Turuhusu huruma yake ijaze mioyo yetu
ili iweze kupokea daima uzuri wa Mungu. Nasi pia kama Yohane, alivyo itwa kuwa
mjumbe wa Ufalme wa Mungu, Yesu anampa kila mbatizwa Roho wake kutangaza kwa
maneno na matendo ufalme wa haki na huruma.
Sala: Bwana, nisaidie niweze kuona dhambi zangu za zamani si katika hali ya
kupoteza tumaini bali kama sababu ya kurudi kwako kwa uaminifu mkubwa. Bila
kujali nimeanguka mara ngapi, nisaidie niweze kunyanyuka na kuimba tena sifa
zako. Yesu nakuamini wewe. Mt. Yohane mbatizaji mhubiri wa ukweli usiye kuwa na
woga, utuombee. Amina
Copyright ©2013-2023 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki:
see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment