Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

WAHUJAJI WA KUELEKEA MBINGUNI!



“KUFUFUKA NA KRISTO”
Tafakari ya Pasaka
Jumapili, Mei 21, 2023. 
Juma la 7 la Pasaka
Sherehe ya kupaa Bwana wetu Yesu Kristo Mbinguni

Mdo 1:1-11
Zab 47: 1-2, 5-6, 7-8, (K)
Ef 1:17-23
Mt 28:16-20


WAHUJAJI WA KUELEKEA MBINGUNI!

Leo Kanisa lina sheherekea sherehe ya Kupaa Bwana wetu Yesu Kristo Mbinguni. Sherehe hii inadhihirisha Umungu wa Kristo, na unasherekewa na wakristo wote. Sherehe hii inadhihirisha kile ambacho tunakiri katika nasadiki “Akapaa mbinguni, ameketi mkono wa kuume wa Baba”. 
Maandiko yanatuambia kwamba Enok na Elia hawakufa, lakini walipelekwa mbinguni. Kanisa pia linatuambia kuwa Bikira Maria alipalizwa mbinguni mwili na roho. Yesu alikuwa Mungu na mwanadamu. Imani yetu ya umwilishi inatuambia kwamba alikuja duniani akapata mwili ili kuwakomboa wanadamu. Yesu sasa anakamilisha utume wake duniani na sasa anapaa mbinguni katika kiti chake cha utukufu milele yote. Kupaa ni mwisho na pia ni mwanzo. Kupaa ni mwisho wa utume wake lakini pia ni mwanzo wa utume wa Roho Mtakatifu. Ni kuvuka katika ngazi nyingine katika mpango kamili wa Baba. 

Mitume huenda walikuwa na hofu na kushangazwa. Yesu alikuwa pamoja nao, alikufa na kufufuka na kuwatokea mara nyingi, na sasa anapaa mbele ya macho yao. Yesu alikuwa ameshawaambia kuwa Msaidizi atakuja na kuwaongoza katika ukweli wote. Mitume watakuwa walitoka katika hofu na kuwa na furaha, kutoka katika huzuni na kuelewa, na kuwa tena na furaha. Pengine ndivyo wengine tunavyo yakuta maisha yetu. Furaha na uchungu, masikitiko na wakati mwingine furaha, nk. Kila tukio hufunua kitu kipya, kitu chenye kutoa changamoto au kuleta utukufu au huzuni. Habari njema ni kwamba mpango wa Baba hujifunua katika ukamilifu wote. Kwa sherehe hii, Yesu anaanza kuelekeza utume wake kwa kuanzisha ufalme wa Mungu kutoka Mbinguni. Ukuu wake ni utawala kama wa kiti cha dereva akielekeza maisha yetu. Kutoka mbinguni Yesu sasa ameanza kushuka katika maisha yetu, akitimiza utume wake kwa njia ya mitume na njia yetu wote. Kupaa haina maana kwamba Yesu ameondoka, bali, ina maana kwamba Yesu yupo sasa kwa kila mmoja wetu anaye mkaribisha na kujikabidhi katika utume wake. Kutoka mbinguni Yesu anauwezo wa kujifunua kwa wote. Yupo tayari kuishi ndani mwetu na kutukaribisha tuishi ndani yake. Ni mwanzo mpya wa Kanisa. Wanacho paswa kufanya sasa Mitume ni kumsubiri Roho Mtakatifu kuwashukia.

Somo la kwanza linaelezea nyakati za mwisho za Yesu mfufuka akiwa na wanafunzi wake hapa duniani. Baada ya ufufuko,Yesu alibaki kwa siku arobaini akiwatokea wanafunzi wake na kuwaongoza. Alikuwa amesahafungua akili zao Kuhusu ujumbe uliomhusu yeye kutoka katika Agano la Kale, lakini kulikuwa bado mambo mengine walio paswa kujifunza zaidi kabla hawaja anza utume wao. Yesu kipindi hicho aliwafundisha mambo mengi kwa ajili ya utume huu maalum. 

Katika somo la Pili Mt. Paulo anaelezea nguvu ya Mungu ya kumfufua Yesu kutoka wafu na kumfanya aketi mkono wake wa kuume, ambapo yeye you juu ya utawala wa vyote, mamlaka na nguvu na tawala. Yesu mfufuka ni Mfalme kweli wa Ulimwengu wote. 

Katika somo la Injili, Bwana kwa mamlaka yote aliyopewa na Baba yake, Yesu ana waamuru wanafunzi wake waende ulimwenguni kote kuwafanya watu wote kuwa wafuasi wake. Anawaita wawe mashahidi wake. Shihidi ni yule anaye shuhudia kile alicho sikia na kuona (Mdo 4: 19-20). Sisi pia tupo kama Wanafunzi wake tunaitwa kumshuhudia na katika mateso, kifo, na kufufuka na kutubu dhambi katika jina la Yesu. Njia pekee ya kushika ukweli wa Yesu mfufuka ni kuwa mashahidi wake popote pale tulipo. 

Wafuasi walitazama juu wakati Yesu alivyokuwa akipaa mbinguni. Sisi nasi tunapaswa kutazama juu, kujikumbusha kwamba maisha yetu hapa duniani ni utume, safari ambayo inakamilika huko mbinguni. Yesu anatuita sisi tupae kwa kwenda katika maisha mengine. Yesu yupo nasi mpaka ukamilifu wa Dahari. Tukaribie sasa kiti cha Mungu cha neema kwa ujasiri, ili tuweze kupokea huruma na kupata neema ya kutusaidia wakati wa taabu (Heb 4:16). Sherehe hii itusaidie tuweze kuishi maisha yetu ya ukristo , kama Enok, Elia na Bikira Maria waliofurahia zawadi ya neema za Mungu. 

Sala: Bwana, katika kila kitu nisaidie kusema “ndio” kwa mpango wako. Ninakuomba nikushuhudie wewe kwa marafiki zangu na jirani zangu kwa njia ya maneno na matendo. Yesu, nakuamini wewe. Amina.


Copyright ©2013-2023 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.

No comments:

Post a Comment