“KUFUFUKA NA KRISTO”
Tafakari ya Pasaka
Jumamosi, Mei 3, 2025
Juma la 3 la Pasaka
Sikukuu ya Mitume Filipo na Yakobo, Mitume
1 Kor 15: 1-8;
Zab 18: 2-5;
Yn 14: 6-14
TUNAITWA KUWA VYOMBO VYA HABARI NJEMA!
Leo tunawakumbuka mitume wa Bwana, Filipo na Yakobo. Yakobo ana barua yake
katika Agano Jipya. Baada ya ufufuko Yesu alimtokea Yakobo ambaye baadae
alienda Yerusalemu na kuongoza Kanisa kwa muda Fulani, na baadae alipigwa kwa
mawe na kufa shahidi.
Filipo ni mtume ambaye anatajwa katika ule muujiza wa kuongeza mikate
katika Injili. Ni yeye aliyevuviwa kumbatiza ofisa wa Ethiopia katika kitabu
cha matendo ya mitume. Mapokeo yanasema kwamba Filipo alihubiri Ugiriki, Frigia
na Syria. Yeye pamoja na Mtakatifu Bartholomeo walisulubishwa miguu juu kichwa
chini. Mapokeo yanatuambia kwamba Filipo aliendelea kuhubiri akiwa amefungwa
pale msalabani miguu juu kichwa chini mpaka alipo kufa.
Yakobo na Filipo waliyatoa maisha yao kwa Kristo, bili kushikilia chochote.
Lakini ilichukuwa muda kukua katika imani na ujasiri katika kumfuata Yesu.
Wanatupa changamoto na sisi tukue kwa kujikabidhi kikamilifu kwa Yesu na
kuamini kikamilifu mapenzi yake.
Ingawaje filipo na Yakobo hawakuwa watu waliojaa Imani mwanzoni. Yesu
hakuwaacha aliwavuta tu kwake, sisi nasi Yesu hatatuacha kama tutaamua
kujikabidhi kwake. Aliendelea kuwaita kwenye utakatifu na huduma takatifu, na
ataendelea kufanya kwetu pia.
Sala: Bwana, ninakushukuru kwa kutokuniacha mimi, hata pale ninapo tenda dhambi
na kwenda mbali nawe. Nisaidie niweze kuvumilia katika Imani yangu kwako na
niweze kujibu wito wako kwa kukufuata kikamilifu popote unapotaka kuniongoza.
Amina
No comments:
Post a Comment