“KUFUFUKA KWA KRISTO”
Tafakari ya Pasaka
Jumatatu, Mei 15, 2023.
Juma la 6 la Pasaka
Mdo 16: 11-15;
Zab 149: 1-6, 9;
Yn 15:26 - 16:4.
ROHO MTAKATIFU: MSAIDIZI
Kanisa lenye msingi wake kwa Yesu linaongozwa na Roho Mtakatifu tangu
Pentekoste. Mtakatifu Paulo na wengine walihubiri Injili ya Yesu. Sehemu yeyote
lilipo hubiriwa neno la Mungu, Roho Mtakatifu ndiye aliyesababisha wongofu wa
mioyo ya watu. Lidia alimsikia Paulo na wengine wakihubiri Injili ya Yesu.
Alifungua moyo wake kwa Bwana. Ina maana kwamba kwanza kabisa alifungua masikio
yake akamsikiliza Yesu, naye Roho Mtakifu akamtia nguvu. Moyo wake na utayari
wake wakukaribisha ujumbe wa Kristo moyoni mwake haukuwa tuu kwaajili yake
binafsi bali ulibadilisha nyumba yake yote.
Wafuasi walimsikiliza Yesu akiwaambia kwamba watafukuzwa katika masunagogi
na hata kuuwawa, maneno haya hawakuyaelewa. Huenda iliwasumbua kidogo, lakini
mara moja kwenda kwa mambo mengine ili wasiyawaze zaidi na kuwasumbua. Na bila
shaka mitume walipo adhibiwa na Mafarisayo na waandishi, waliyakumbuka maneno
haya ya Yesu. Walitambua walipaswa wawaongoze kwenda kwa Mungu, wana sababisha
adha katika maisha yao. Watakuwa walijaribiwa katika hali ya kutaka wapoteze
Imani yao. Lakini Yesu alitabiri jaribu hili kuu litakuja, lakini akawaonya na
kuwaambia kuwa yatakuja.
Lakini kinacho vutia ni kile ambacho Yesu hakusema. Hakuwaambia kwamba
watapigana na kurudisha, kuanza fujo, au mapinduzi yeyote nk. lakini tunamuona
Yesu akiwaaambia Roho Mtakatifu ndiye atakaye shughulika na hayo. Atawaongoza
na kuwawezesha kumshuhudia Yesu. Kuwa mkristo maana yake umekubali mateso.
Roho Mtakatifu anaitwa “Msaidizi”, huwafariji waamini, hasa wakati
wauhitaji na mateso. Pia, wakati mwingine kile tunacho dhani ni ukweli kinaweza
kisiwe ni ukweli kabisa, kinaweza kuchanganywa na uongo. Yeye pia ni “Roho wa
Ukweli”, anayetuonyesha ukweli- kwamba ni Yesu aliyesema ‘mimi ni ukweli, njia
na uzima’ (Yn 14:6). Leo tujiulize kama maisha yetu yanaongozwa na Roho
Mtakatifu?
Sala: Bwana, ninapo elemewa na mzigo wa ulimwengu au mateso nipe Amani ya
mwiili na Roho. Ninaomba unipe nguvu kwa uwezo wa Roho Mtakatifu ili niweze
kuwa shahidi wako. Yesu, nakuamini wewe. Amina.
No comments:
Post a Comment