“KUFUFUKA NA KRISTO”
Tafakari ya Pasaka
Jumapili, Mei 14, 2023.
Dominika ya 6 ya Pasaka
Mdo 8: 5-8, 14-17;
Zab 65: 1-7, 16, 20;
1 Pet 3: 15-18;
Yn 14: 15-21.
ROHO MTAKATIFU, MSAIDIZI!
Kwa, jumapili ya sita ya Pasaka tunaanza kufungua macho yetu na kuanza
kutazamia ujio wa Roho Mtakatifu. Yesu anaongea kuhusu kumuomba Baba alete
msaidizi mwingine awe nasi daima. Huyu msaidizi ni Roho Mtakatifu.
Katika somo la kwanza tunasikia kuhusu Filipo. Anafika Samaria na anaanza
kuhubiri Injili na kubatiza wote waliopokea Imani. Roho Mtakatifu aliwaimarisha
wamisionari hawa wa kwanza kwa kuwapa nguvu katika maneno yao kwa kudhihirisha
uwepo wake kwa ishara. Watu wa mji ule walibadilika na wakajazwa na furaha.
Sehemu ya pili ya somo inamuonesha Petro na Yohane wakiwatembelea wabatizwa
huko Samaria. Mitume hawa wawili waliwawekea mikono ili Roho Mtakatifu aweze
kuwa juu yao. Walishangazwa Wasamaria waliobatizwa na Filipo walikuwa
hawajapokea Roho Mtakatifu. Uwepo wa Mungu ulikosa ishara ya njee ambayo
ilikuwepo wakati wa Kanisa la mwanzo. Luka anaunganisha matukio haya mawili,
kutuonesha kwamba kila sehemu Injili ilipo hubiriwa kuna jumuiya mpya
inayokuwa. Lakini, hawakuhitaji kukuwa, kuendelea na kuishi katika hali ya
pekee kabisa na inayo jitegemea. Ni vizuri walianzisha umoja wa kuunganisha na
kanisa nzima. Ni Roho pekee atakaye jidhihirisha ndani yao wote.
Katika somo la Injili tunaona ujumbe wa wosia wa Yesu. Mitume wanahuzuni
kwababu ya kuondoka kwa Yesu, na wana ahidiwa msaidizi mwingine Yesu anaeleza
wazi kwamba Roho Mtakatifu watampokea tu wale waIe walioungana naye, katika
mipango yake na katika kazi zake za upendo. Huyu Roho anaitwa kwa majina
mawili. Mfariji na Roho wa kweli.
Msaidizi ni neno linalo onesha kwamba ni yule aliyeitwa ili aweze
kuambatana. Hapo kale kulikuwa hamna kuanzishwa kwa sheria, kila mtu alipaswa
kujitetea na kujilinda mwenyewe. Ilitokea mara chache kwamba, mtu hana kosa,
lakini mtu haweze kudhihirisha kwamba hana hatia. Kwake kilicho salia ni
tumaini moja tu: kwamba mtu mmoja wa heshima atatokea katika mkutano aongee
bila kusita na kutoa ushahidi wa kumtetea. Ishara hii ni sawa na kufunguliwa
gerezani. Na wala hakuna yeyote atakaye kushutumu tena. Huyu anaitwa “Msaidizi”
maana yake yule anayeitwa ili aweze kuwa karibu na mwingine ambaye amepata
matatizo. Yesu aliwahidia wafuasi wake msaidizi, kwasababu tayari wamesha mpata
wa kwanza ambaye ni Yesu mwenyewe. Roho Mtakatifu ni Msaidizi kwasababu
anawasaidia Wafuasi katika vita dhidi ya malimwengu hasa maovu. Yohane
anawakumbusha wafuasi juu ya ukweli huu ili wanapo kutana na ugumu katika
maisha, wasikatishwe tamaa, kupoteza tumaini, bila kupoteza Amani ya moyo na
furaha. Wafuasi waliamini juu ya usaidizi wa Roho Mtakatifu. Wana amini nguvu
ya Msaidizi huyu na kwamba hatashindwa.
Roho wa ukweli anafanya kazi katika huduma ya kweli. Ujumbe wa Yesu
umeelekezwa kwa watu wote. Unapaswa kuhubiriwa mpaka miisho ya ulimwengu. Roho
Mtakatifu anadhihirisha kwamba hatashindwa, na wala hayata fafanuliwa vibaya na
kuharibiwa, mafundihso ya Kristo. Yeye haondoi tu makosa yanayo fanywa na
kukosewa katika kurithisha ujumbe wa Yesu. Anawatambulisha wafuasi katika
ukweli wote. Yeye yupo katika kuwaelekeza wafuasi katika kutambua ukweli wote.
Hatasema kitu kingine kipya kinacho pinga ujumbe wa Yesu. Atasaidia katika
kuendeleza ujumbe wa Yesu mpaka miisho yote. Kazi ya Wakristo nikubaki imara
katika kazi hii ya Roho Mtakatifu ambaye daima anafunua mambo mapya. Yeye kwa
asili ndiye anaye ufanya upya uso wa Nchi (104:30). Ni dhambi juu ya Roho
Mtakatifu kupinga kufanywa upya, kukataa kufanya mabadiliko katika maisha ya
jumuiya, ambayo yanawaleta watu karibu na Yesu na wandugu, ambayo huongeza
furaha na amani ambayo yanawafanya watu wasali vizuri na kufanya moyo uwe huru
na kuondoa hofu zote.
Kama tupo wazi kwa ujio wa Roho Mtakatifu, tutapokea Msaidizi mzuri kabisa
katika maisha yetu yote. Roho Mtakatifu ndiye msaidizi tunaye mhitaji. Kuzama
ndani ya Roho Mtakatifu inatufanya tujazwe na neema zote katika maisha. Sali
sala ya Roho Mtakatifu na kutarajia kusherekea dominika ya Pentekoste jumapili
mbili zijazo.
Sala: Ee, Mungu, wewe ambaye kwa Roho Mtakatifu, unaongoza Roho za Waamini
wako, jalia kwa Roho huyo huyo, tuweze kuwa wakweli na wenye hekima na
kufurahia faraja yake, kwa Njia ya Kristo Bwana wetu. Yesu, nakuamini wewe.
Amina.
No comments:
Post a Comment