“Atakapokuja huyu Roho wa kweli
, atawaongoza kwenye ukweli wote” (Yn 16:13)
Baada ya kusema hayo, Yesu
aliinua macho yake kuelekea mbinguni akasema “Mimi nimekutukuza hapa duniani;
nimeikamilisha kazi uliyonipa niifanye. Naomba ili wote wawe kitu kimoja kusudi
ulimwengu upate kuamini kwamba Wewe ulinituma (Yn 17:4,21).
Nasi twamuomba Mungu Mwenyezi
alijalie kanisa lake umoja wa kweli, awaunganishe wakristu wa madhehebu yote
katika zizi moja chini ya mchungaji mmoja.
Popote duniani watu wengi,
makundi kwa makundi wanavutwa na neema hiyo ya kuungana na kuufikia umoja wa
Kanisa. Hata ndugu zetu waliotengana nasi wanazidi kukubali mwongozo wa Roho
Mtakatifu na kutaka kurudi katika nyumba ya Baba na kuwa kundi moja chini ya
mchungaji mmoja. Isitoshe, hata sasa tena twaweza kuona kwamba kwa namna fulani
wamejiunga nasi katika Roho Mtakatifu, naye Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani
yao kumshuhudia hata kwa kumwaga damu yao.
Tena katika hao ndugu zetu
waliojitenga, Roho Mtakatifu analisha katika mioyo yao ile ya imani
inayowaunganisha wafuasi wote wa Kristu. Tumwombe basi Mwenyezi Mungu atujalie
hima huo umoja wa Kanisa lake tunaouania mno.
1. Ee Yesu Bwana wetu wewe umetuombea kwa
Mungu Baba tuwe itu kimoja kama Wewe ulivyo kitu kimoja na Baba. Utujalie huo
umoja, ili ulimwengu uone na kukiri kwamba ndiwe Bwana na Mkombozi wa watu wote
W. Twakuomba utusikie
2. Ee Yesu utujalie moyo wa kulishika neno
lako kwa uaminifu, wala usituache kufuata njia zetu sisi wenyewe na kufarakana.
W. Twakuomba utusikie
3. Ee Yesu uliye Mchungaji wetu mwema,
ondoa ndani yetu ile tabia ya utengano, tupate kuwa sote kundi moja chini yako
wewe uliye mchungaji wetu mmoja.
W. Twakuomba utusikie
4. Ee Yesu, uliye Mchungaji mkuu, uwajalie
wachungaji wetu wawe siku zote na upendo wa Jina lako, wasichoke kulichunga
vema kundi lako hapa duniani na kuliweka pamoja lisitengane
W. Twakuombaa utusikie
5. Ewe Roho Mtakatifu, uziangaze akili za
watu wote, wapende siku zote kuishi kwa amani, umoja na mapendano
W. Twakuomba utusikie
6. Ee Mungu, utufungulie …… wa muungano
wako wa kweli sisi tulio ndugu katika Bwana wetu Yesu Kristu.
W. Twakuomba utusikie
7. Utujalie mapatano na amani, tudumu
tumeungana katika familia zetu, katika jimbo letu na katika nchi yetu yote.
W. Twakuomba utusikie.
TUOMBE;
Ee Mungu, utuunganishe sisi
kondoo wako tuliotawanyika, tuwe chini ya Mwanao mpenzi, tupate sote kuushiriki
ule utawala wako wa kweli na haki, utawala wa neema na amani, utawala wa upendo
wako. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu
No comments:
Post a Comment