“KUFUFUKA NA KRISTO”
Tafakari ya Pasaka
Ijumaa, Mei 5, 2023,
Juma la 4 la Pasaka
Mdo 13: 26-33;
Zab 2: 6-11;
Yn 14: 1-6.
MBINGUNI NI NYUMBANI KWETU!
Mara kwa mara ni muhimu kuweka jitihada kuelekea kwenye utukufu wa
Mbinguni! Mbingu ipo na ni mapenzi ya Mungu sisi wote siku moja tufurahi na
Utatu Mungu mmoja. Kama tunatambua kwa hakika kuhusu mbingu, tunakuwa tunaitamani
kwa moyo wote na tunawaka mapendo na kuitazamia kwa nguvu kubwa, tukiwa
tumejazwa na Amani na furaha kila wakati tuki ifikirie. Kwa bahati mbaya,
habari za kuacha ulimwengun huu na kwenda kukutana na Muumba wetu kwa wengi
zina ogopesha. Pengine ni hofu ya mambo yasio julikana, utambuzi wa kwamba
tutawaacha wapendwa wetu, au hofu ya kwamba huenda tusiende mbinguni.
Kama Wakristo, ni vizuri kujishughulisha tukitambua upendo wetu mkubwa
mbinguni kwa kupata utambuzi mkubwa wa sio mbinguni pekee, bali kutambua jukumu
la maisha yetu hapa duniani. Mbingu inasaidia sisi tuweze kupanga maisha yetu
kwa kupitia ile njia inayo tuongoza kwenye heri hiyo. Katika Injili, tunapewa
picha nzuri sana yenye kufariji kuhusu Mbinguni, ambayo ni “Nyumba ya Baba”.
Nyumbani ni sehemu salama. Ni sehemu ambayo tunaweza kufurahia na kuishi bila
kujifanya, kuwa na wapendwa wetu, kupumzika, na kujisikia ni sehemu ya familia.
Sisi ni watoto wa Mungu na hivyo Mungu anapenda sisi tuwe nyumbani pamoja naye.
Kwa kutafakari juu ya picha hii, inapaswa pia iwe faraja kwa wale wote
waliopoteza wapendwa wao. Hali ya kusema kwaheri, ni ngumu. Na inapaswa kuwa
ngumu. Ugumu wa kupoteza wapendwa wetu inaonesha uwepo wa upendo wa kweli
katika mahusiano. Lakini Mungu anapenda hali ya hisia za kupoteza wapendwa wetu
ichanganyike na furaha tunapo tafakari ukweli wa wapendwa wetu kuwa wapo na
Baba nyumbani milele. Wana furaha kule zaidi ya jinsi tunavyo weza kudhania, na
siku moja nasi tutaitwa kushiriki furaha hiyo.
Sala: Bwana, natamani daima kuwa nawe. Nisaidie daima niweke lengo hili
daima akilini mwangu, na kukuwa nalo siku zote kwa tamaa ya kufurahi nawe milele.
Yesu, nakuamini wewe. Amina.
No comments:
Post a Comment