“KUFUFUKA NA KRISTO”
Tafakari ya Pasaka
Kumbukumbu ya Mt. Atanasi (Askofu)
Jumanne, Mei 2, 2023,
Juma la 4 la Pasaka.
Mdo 11:19-26;
Zab 87:1-7 (R. 117:1);
Yn 10:22-30
IMANI NI LUGHA YA KUMFAHAMU MUNGU!
Katika somo la kwanza Barnaba anaona Roho Mtakatifu akifanya kazi ndani ya
watu wa Antokia na hivyo anawatia moyo na kuwapa nguvu “Wakristo”. Katika somo
la Injili, Wayahudi wanakataa kumkaribishi Yesu. Wanamuuliza “kama wewe ni
Kristo tueleze wazi”. Na Yesu anajibu kwamba, “nime waambia lakini
hamkusadiki”. Je wewe unasadiki Yesu ni nani kwetu? Je tupo wazi kwa kazi ya
Roho Mtakatifu?
Pengine umemtaka Mungu ashuke kutoka mbinguni aje akupe majibu wazi ya
kwanini baadhi ya mambo yapo kama yalivyo au kama yanavyo tokea? Au kukupa
majibu wazi ya maswali yako. Lakini hafanyi hivyo. Anafanya hivyo katika hali
ya njia yake kamili kwa lugha yake kamili. Ni kwa lugha ya Imani na hii
inahitaji kujikabidhi kwa Mungu kabisa na mapenzi yetu yote ili tuweze kusikia na
kuelewa. Hii ndio njia ya kweli ya kuongoka na kuwa katika njia ambayo Mungu
anataka sisi tuwe. Tukitegemea akili na utashi wetu wenyewe, tutashindwa kuona
uwepo wa Mungu, na kama tutataka akili yetu itoe majibu yote, ni wazi kwamba
tutafikia mahali pakuona hamna haja ya Mungu kwasababu tunajitosheleza kwa
akili zetu. Imani yaweza kutupa majibu ambayo akili zetu haziwezi kutambua.
Sala: Bwana, mara nyingi nimeshindwa kukusikiliza wewe na kukuelewa kwa
njia ya zawadi ya Imani. Mara nyingi nimependa kupata majibu marahisi kwa
maswali magumu. Nisaidie niweze kukuwa katika uvumilifu ili niweze kukufahamu
na kukuruhusu kuwa Mchungaji wangu. Yesu nakuamini wewe. Amina
No comments:
Post a Comment