“KUFUFUKA NA KRISTO”
Tafakari ya Pasaka
Alhamisi, Mei 18, 2023
Juma la 6 la Pasaka
Mdo 18: 1-8;
Zab 98: 1-4;
Yn 16: 16-20
FURAHI KATIKA BWANA!
Bwana wetu katika Injili, anawaambia Wanafunzi wake kwamba bado kitambo
kidogo watamwona na bado kitambo kidogo hawatamwona. Aliwaandaa kwa kifo na
ufufuko wake. Anawaambia watalia na kuhuzunika wakati ulimwengu utakuwa
ukifurahi, bali huzuni yao itabadilishwa na kuwa furaha. Kwahiyo wakati
walivyokuwa wanamuona Bwana baada ya ufufuko ilikuwa nikukamilisha unabii juu
yake. Kwa upande wa Ulimwengu itakuwa kinyume, furaha ya ulimwengu itageuka
kuwa huzuni.
Yesu anawaambia wanafunzi wake kwamba huzuni na furaha itakuwa sehemu ya
maisha yao ya kila siku. Ni kitendo cha upendo kwa upande wake, kuwa mbele ya
wanafunzi wake kuhusu magumu watakayo kutana nayo mbele. Habari njema ni kwamba
Yesu anasema usemi huu ukifuatana na usemi wa matumaini kwamba “huzuni yao itageuka
kuwa furaha”. Ni wazi pia katika maisha yetu. Yesu hatupi ahadi kwamba maisha
yetu yatakuwa ya furaha tuu bila magumu na huzuni. Hatuambii kwamba kumfuata
yeye, kila kitu kitakuwa shwari na rahisi. Kama tutafuata njia zake tuwe tayari
kuona magumu na uchungu ambayo ndio njia itakayo geuka na kuwa neema na furaha
kwa wengi. Kama tutaweze kukabili magumu ya maisha kwa imani na matumaini,
hakuna kitakacho tuweka chini na kila kitu kitaweza kutumika kwa utukufu wa
Mungu na yataishia katika furaha kubwa.
Kilicho cha muhimu kwetu nikubaki tukiwa tunamwelekea Bwana kwasababu ni
kutoka kwake na ni kutoka kwake upendo wote watoka, na ni kutoka kwake furaha
yote yatoka. Furaha inayotokana na ulimwengu ni fupi na ya muda tu, tena
inayopita. Hakuna kitu kinacho baki milele kinacho tokana na ulimwengu. Furaha
inapatikana kwa Yesu pekee. Usihuzunishwe wala kukatishwa tamaa wakati maisha
yanakuendea vibaya. Usipoteze matumaini wakati magumu yanapo tokea katika
maisha yako. Kabidhi kila kitu kwa Bwana wetu na muache avigeuze viweze kuwa na
furaha ile aliyoahidi mwishoni.
Sala: Bwana, ninakabidhi mateso yangu yote ya maisha yangu, mikonini mwako.
Huzuni, magumu, mateso na kuchanganyikiwa nina jikabidhi mikononi mwako. Nina
amini kwamba wewe ni mwenye nguvu na unatamani kubadili vyote katika utukufu
wako. Nipe matumaini wakati wa kupoteza matumaini na kukutegemea wakati maisha
yakiwa magumu. Yesu, nakuamini wewe. Amina
No comments:
Post a Comment