Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

UHUSIANO WETU NA MUNGU

“KWARESIMA YA UKARIMU”
Tafakari ya Kwaresima
Jumanne, Machi 28, 2023
Juma la 5 la Kwaresima

Hes 21: 4-9;
Zab 101: 2-3, 16-21; 
Yn 8: 21-30.


UHUSIANO WETU NA MUNGU


Katika somo la kwanza tunasikia waisraeli wakimlalamikia Mungu na Musa. Hawa watu walikombolewa kutoka utumwani, lakini wanataka tu kurudi tena huko utumwani. Hawaku mfahamu Mungu, aliye wakomboa. Hawakuwa na uhusiano wa kweli naye. Katika somo la Injili tunamuona Yesu anavyo jali, na upendo wake kwa wanadamu. Karne baada ya karne waliwasikia manabii, na walitegemea Masiha. Lakini aliposimama kati yao walishindwa kumtambua. Uelewa wao kuhusu Masiha haukuwa kamili. Yesu anajaribu kuwaamsha kwa mafundisho yake. 

Baba ndiye aliye mtuma Yesu ulimwenguni kwa utume na Yesu anakiri kwamba Mungu hawezi kumwacha. Yesu anatambua hili na anafurahia Baraka za Kimungu kwa muunganiko huu. Tofauti na Waisraeli na mafarisayo, Yesu anatambua uhusiano wake na Baba.

Sisi tunaweza kuwa “Wakristo walio lala”. Tunafahamu kusali, tunafahamu ni muda ghani wa kusimama, wakati wa kupiga magoti, wakati wa kukaa tukiwa kanisani, lakini uhusiano wetu na Mungu ni wakati tu tukiwa na furaha. Tunaanza kuwa na wasi wasi na Mungu tunapo kumbani na Matatizo. Liturjia ya leo inatutaka tuwe wakristo tulio amka, kuwa na uelewa na uhsiano wetu na Mungu na pia kuelewa mambo ya ulimwengu. Yesu kwa sadaka yake msalabani ametukomboa kutoka katika utumwa wetu wa dhambi. Kipindi hichi cha kwaresima tunaitwa kuwa wapya katika mapendo na Mungu, kumgeukia Yesu msalabani na kutafuta upendo, msamaha na huruma kutoka kwake, na kuwa upendo na huruma kwa wengine. 

Tafakari leo juu ya utume aliopewa Yesu: maisha yake ya kujitoa sadaka. Tafakari jinsi Mungu anavyopenda tuishi utume huu kwa maisha ya sadaka ya upendo na kujitoa. Unaweza kuwa uyaishi kwa moyo wako wote, au unaweza kuwa unahitaji kuelekezwa upya. Sema “ndio” kwa mapenzi yake kwa ujasiri na ushujaa na Mungu atatembea nawe katika kila hatua ya maisha yako. 

Sala: Bwana, ninasema “ndio” kwa mpango kamili ulionao katika maisha yangu. Vyovyote itakavyokuwa ninakubali bila kuwa na mashaka, Bwana mpendwa. Ninatambua upo na mimi daima na sipo mwenyewe. Yesu nakuamini wewe. Amina

Copyright ©2013-2023 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.

No comments:

Post a Comment