“KUFUFUKA NA KRISTO”
Tafakari ya Pasaka
Jumatano, Aprili 19, 2023
Juma la 2 la Pasaka
Mdo 5:17-26
Zab 34:2-9
Yn 3:16-21
KUVUTWA KWENYE MWANGA!
Mungu Baba amemtuma Mwanae aje ulimwenguni kuwa mwanga wetu wote. Yeye ni
Mwanga ambao unaondoa giza lote. Lakini Injili inasema kwamba “watu wamependa
giza zaidi ya mwanga”. Wamechagua dhambi zao zaidi kuliko uhuru wa kutoka
kwenye dhambi. Tv au magazeti huvutia watu zaidi wanapotoa habari za udhaifu wa
watu, na watu hukimbilia hizi kwasababu ndicho chenye maana kwao. Kwasababu
tunavutwa zaidi kupenda kusikia mambo ya giza kuliko ya mwanga.
Ni wazi kwamba sio kwa kila mtu. Walio wengi hawapendezwi na giza la
ulimwengu pia na mambo ya kudhalilisha wengine. Lakini ukweli ni kwamba giza
lipo mbele na tunapaswa kuwa makini kwasababu ya hali yetu yakuweza kuanguka.
Tunapenda kwenda kwenye matope na kudhani tuna furaha.
Pasaka ni kipindi cha kuchunguza tunavutwa na nini zaidi. Je, tunajiruhusu
sisi wenyewe kuvutwa kwenye mwanga? Je, tunavutwa na hali mbali mbali ambazo
Mungu yupo karibu yetu hapa duniani? Lakini upo mvuto wa kutopenda mpangilio,
nakuvutwa kwenye dhambi, mapambano ya ndani ambayo kila mtu yanamkuta. Pasaka
ni kipindi cha kuwa makini na haya, kuya chunguza na kuyaona na kuamua
kumchagua Yesu, kuanza kujenga maisha yetu ya fadhila kwa kuiga fadhila za
maisha ya Yesu.
Kama wafuasi wa Yesu tunaitwa kuelekeza macho yetu kwake pekee. Tunapaswa
kupenya giza kwa Imani na kuacha mambo yetu yavutwe kwa Yesu Kristo. Tujikite
kwenye Mwanga katika kipindi hiki cha Pasaka. Tuache mwanga huu uongoze maisha
yetu.
Sala: Nisaidie mimi niweze kuishi kwenye mwanga. Nisaidie niweze kuelekeza
macho yangu kuelekea kwenye utukufu wa ufufuko wako. Ninaomba furaha hiyo iweze
kuondoa uharibifu wa mabaya ndani mwangu. Yesu, nakuamini wewe. Amina.
No comments:
Post a Comment