“KWARESIMA YA UKARIMU”
Tafakari ya Kwaresima
Ijumaa, Machi 1, 2024
Juma la 2 la Kwaresima
Mwa 37:3-4, 12-13, 17-28;
Zab 105:16-21;
Mt 21:33-43, 45-46
UPENDO UNAOTESEKA
Katika njia nyingi, Yusufu alikuwa mwaminifu, alikuwa akilindwa katika
upendo na kutendewa vyema na Baba yake. Lakini kutokuwa na hatia kulimweka
mashakani mara pale alipowaambia ndugu zake kuhusu ndoto yake, na
alipowaonyesha kanzu nzuri Baba yake aliyokuwa amempa. Baadaye, ingawa ndugu
zake walimpiga na kumuuza utumwani, Yusufu hakuacha kuziishi amri za Mungu.
Hata alipokuwa ameshtakiwa kwa uongo na kufungwa gerezani kwamba alijaribu
kumwingilia mke wa bwana wake kwa nguvu, yeye aliendelea kuwa imara mbele ya
Mungu. Wakati akiwa gerezani, uwezo wake wa kutafsiri ndoto ulimfikia Farao
ambaye hatimaye alimweka huru na kumweka awe mkuu baada yake. Kama Yusufu
alivyoamini kwamba, Mungu atamletea mema, Mungu alifanya hivyo kwa ajili yake
na kuutenga uovu. Nasi pia, tusikubali kamwe kumuacha Mungu tunapokabiliana na
magumu siku zote katika maisha yetu. Tumgeukia Mungu Baba yetu na kumwomba
atupiganie.
Katika hali zote za kuchukiwa na kukataliwa kwa karne zote, kuna mmoja tu
aliyesimama imara kuliko wengine wote. Kukataliwa kwa Mwana wa Mungu. Yesu
hakuwa na kitu kingine isipokuwa upendo kamili moyoni mwake. Alipenda ubora wa
kila aliyekutana naye. Na alikuwa tayari kumpa upendo yeyote aliyekuwa tayari
kuupokea. Ingawaje wengi waliupokea lakini pia wengi waliukataa. Ni vizuri
kutambua kuwa kukataliwa kwa Yesu kuliacha maumivu ya ndani na mateso. Ni wazi
kwamba mateso ya Msalabani ndio yaliokuwa ya hali ya juu kabisa. Lakini kidonda
alichohisi moyoni mwake kwa kukataliwa kilisababisha mateso makubwa. Kuteseka
namna hii ilikuwa ni kitendo cha upendo, sio kitendo cha udhaifu. Yesu
hakuteseka ndani kwasababu ya majivuno au kwasababu ya ubinafsi wake. Bali moyo
wake uliumia kwasababu alipenda kutoka ndani. Na pale upendo huo ulipo
kataliwa, ulimjaza yeye huzuni kuu (Mt 5:4).
Jaribu kufikiria kama Yesu ange amua kukata tamaa. Jaribu kufikiria, kama
kipindi cha kukamatwa kwake Yesu angeita malaika kama jeshi kutoka mbinguni
kumwokoa. Ingekuwaje kama angefanya kitendo hichi cha kufikirika “watu hawa
hawastahili!”. Matokeo yake yangekuwa tusinge pokea zawadi ya ukombozi wa
milele kwa njia ya mateso, kifo na ufufuko. Mateso yasinge badilika kwenda
kwenye upendo.
Yesu alijibu kwa mapendo kamili pale alipolia kwa sauti kuu “Baba,
wasamehe, hawajui watendalo.” Kitendo hiki cha upendo katikati ya mateso yake
na kukataliwa kwake kilimfanya awe “jiwe kuu la msingi” la Kanisa, na hivyo
kuwa jiwe kuu la maisha mapya! Tunaitwa kuiga mapendo haya na kushiriki sio tu
kwakusamehe, bali pia kutoa mapendo matakatifu ya huruma. Tukifanya hivyo, sisi
pia tunakuwa jiwe la msingi la upendo na neema kwa wote wanao hitaji zaidi.
Sala: Bwana, nisaidie mimi niweze kuwa jiwe la pembeni. Nisaidie mimi sio
nisamehe tu kila mara ninapokosewa bali pia nitoe upendo na huruma kwao. Wewe
ni Mungu na mfano kamili wa upendo huu. Ninaomba nishiriki katika upendo huu,
nikilia kwa sauti kuu pamoja nawe “Baba wasamehe, hawajui watendalo”. Yesu,
nakuamini wewe. Amina.
No comments:
Post a Comment