“KWARESIMA YA UKARIMU”
Tafakari ya Kwaresima
Jumapili, Machi 12, 2023
Juma la 3 la Kwaresima
Kut 17: 3-7;
Zab 95: 1-2, 6-9;
Rum 5: 1-2, 5-8;
Yn 4: 5-42.
UNA KIU?
“Gods must be crazy” Ni jina la
filamu na ni juu ya watu walioko katika Jangwa la Kalahari. Filamu hii
inaonesha wazoefu wa jangwa. Mmoja wa watu hawa alitembelea mabubujiko ya maji
ya Tungela (maporomoko makubwa ya maji Afrika), huko Afrika kusini. Alishangazwa
kuona maji makubwa yanashuka kutoka juu. Alisimama pale kwa masaa akishangaa.
Hawa watu waliopo Kalahari walizoea kukusanya maji kutoka katika majani
(umande) au kupata maji kutoka katika aina ya mmea ambao shina lake huwa na
maji, ili kupooza kiu yao. Kama ilivyo katika simulizi hilo, lirtujia ya leo ya
Domini ya tatu ya Kwaresima inatuonesha kwamba sisi wote tuna kiu. Watu wana
kiu ya fedha, anasa, madaraka, na mali, na hata kama akipata nyingi, bado kiu
ni kubwa. Katika hali nyingine kuna “maji ya uzima” upande mwingine ndani ya
Yesu Kristo. Tunapojiandaa wenyewe kuingia katika mafumbo ya mateso, kifo na
ufufuko wa Bwana wetu Yesu Kristo kipindi hiki cha Kwaresima, tunaitwa leo
tutulize kiu yetu ya kiroho na kutuliza kiu ya Yesu anayezitafuta roho zetu na
ana zisubiri zirudi kwake. Yesu alipata kiu ya mwanadamu kumrudia Mungu, na
hivyo akasema pale msalabani “Nina kiu”.
Katika somo la kwanza
tunaona Waisraeli wanao lalamika. Watu hawa hawa waliovushwa salama kutoka
katika utumwani huko Misri, na waliokuwa wakitembea kwa uhuru kuelekea Nchi ya
ahadi. Kwanza kabisa walilalamika kuhusu chakula, Mungu akawapa mana, mkate
kutoka mbinguni. Hata baada ya kuona muujiza huu bado hawaja uamini upendo wa
Mungu. Wakaanza kukusanya zaidi ya mahitaji yao, lakini yote iliharibika siku
iliofuata. Alafu wakaanza kulalamika kwasababu ya maji. Pamoja na hilo Mungu
akafanya muujiza mwingine akawapa maji. Lakini Israeli hakujifunza kumtuminia
Mungu. Mwanadamu ni kiumbea ambaye haridhiki. Mahitaji yetu daima tunaona hayatoshi,
yanaendelea kuongezeka daima. Ni kama vile kula chumvi, unahisi kiu kila
wakati, alafu baadae unakula tena chumvi unahisi kiu tena.
Katika somo la Injili tunamuona huyu Mwanamke msamaria ambaye pia alikuwa
akiishi maisha yake yasio pendeza. Alikuwa katika kisima ili kutuliza kiu yake
ya kila siku. Alikuwa anajiribu kutuliza kiu ya mwili wake kwa kila aina ya
anasa. Lakini kila siku alikuwa akirudi katika kisima kwa ajili ya maji. Yeye
kama ilivyo kwa wanadamu wote ni lazima alisimama nakuuliza “hivi kuna aina ya
maji ambayo nikinywa sintaona kiu tena?”. Mt. Agustino anatoa jibu anavyosema
“mioyo yetu haitatulia …hadi itakapo tulia kwako Bwana Yesu”
Yesu alikuwa njiani kuelekea Yerusalemu kwa kupitia Samaria. Watu wasamaria
walionekana kama Wayahudi wasio faa au Wayahudi waliochanganyika. Hawakuwa
wakichukuliwa kama sehemu ya jamii ya Wayahudi. Hata tunaona Yesu anakutana na
Mwanamke Msamaria. Huyu Mwanamke alikuja katika kisima kuja kuchota maji saa
sita mchana. Hii ilikuwa sio kawaida kwasababu, wanawake walikuja kuchota maji
wakiwa katika makundi tena ikiwa ni hasubuhi au jioni. Huyu mwanamke inaonekana
alipenda kuwakwepa wenzake pengine kwasababu ya tabia ya maisha yake ambayo
Yesu alimwambia baadae. Yesu akiwa ni Myahudi anamuomba maji ya kunywa. Alikuwa
na mazunguzo naye ambayo yalimlenga kutoka katika mazungumzo ya maji ya kawaida
hadi kwenye maji ya uzima, kutoka katika kiu ya kidunia hadi kiu ya kiroho.
Anashindwa kumtambua Yesu hapo mwanzo, na Yesu anirarua dhamiri yake kwa
kufunua ukweli wa maisha yake. Hili lilikuwa rahisi kwake kupokea neema ya
Mungu. Yesu anamsaidia katika hali ya kukuwa na kutambua kumwadudu na hapo
anamtambua Yesu kama Masiha. Baada ya kumtabua Yesu, analeta kijiji kizima
kwake. Mwanamke ambaye alikuwa amekataliwa na jamii anakuwa chombo cha Mungu
cha kuwaleta wanakijiji kwa Yesu. Alikuja kuchukua maji ya kawaida akarudi na
maji ya uzima. Yesu hakunywa hata tone moja la maji, lakini kiu yake ilitulizwa
kwa kupata roho moja kwa ajili yake.
Yesu alijua yote kuhusu huyu Mwanamke lakini alitaka kumpa maji ya uzima.
Alitaka kuzima kiu ambayo yeye alikuwa nayo rohoni mwake. Alivyokuwa akiongea
naye, na kuanza kumsikiliza kiu yake ilianza kuzimwa. Ilianza kuzimwa kwasababu
ndicho alichohitaji, tunachohitaji wote, ni upendo huu kamili na kukubaliwa na
Yesu, ambao Yesu anautoa mwenyewe. Alitoa kwake, na anataka kuutoa kwetu pia.
Cha kushangaza Mama huyu aliondoka na kuacha “mtungi”. Hakuchukua maji aliokuwa
amekuja kuchukua. Au alichukuwa? Katika hali hii ya kuacha mtungi ni alama
kwamba kiu yake ilikuwa imezimwa kwa kukutana na Yesu. Hakuwa tena na kiu, Yesu
alizima kiu yake.
Katika kuishi kwetu kila siku, tunajikuta tukimwacha Mungu na kutafuta
mambo yanayo pita. Tunafatilia tukitafuta maana katika hivyo vitu lakini
tunakuta hamna, ni utupu ndani yake. Tutafakari juu ya kiu isiopingika tulio
nayo ndani mwetu. Tukisha itambua, tuelekeze dhamiri zetu kumwelekea Yesu ili
azime kiu yetu kwa maji ya uzima. Tukifanya hivi, tutaacha mitungi mingi ambayo
kwakweli haizimi kiu yetu.
Sala: Bwana, wewe ni maji ya uzima ambayo roho yangu inatafuta. Ninakuomba
nikutane na wewe katika maisha yangu, katika aibu yangu na maumivu ya moyo.
Ninaomba nikutane na upendo wako, upole wako na kukukubali sasa, ninaomba
upendo wako uwe chanzo cha maisha yangu ndani yako. Yesu nakuamini wewe. Amina.
No comments:
Post a Comment