Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

MSAMAHA


“KWARESIMA YA UKARIMU”
Tafakari ya Kwaresima
Jumanne, Machi 14, 2023,
Juma la 3 la Kwaresima

Dan 3:25,34-43;
Zab 25:4-9;
Mt 18:21-35


MSAMAHA


Injili ya leo inatupa mfano wa jinsi ya kupokea na kutoa msamaha. Kinachovutia, ni rahisi kusamehe zaidi ya kuomba msamaha. Kwakweli katika kuomba msamaha inahitaji kuwa mwaminifu kwanza kwa kukubali kwamba nimekosa, ambapo mara nyingi ni jambo ngumu kulifanya. Ni vigumu kuchukua jukumu kwa lile tulilokosa. Katika mfano huu, huyu mtu anayeomba apewe muda ili aweze kulipa anaonekana kuwa mwaminifu. “Anapiga magoti” mbele ya Bwana wake kwa huruma na kuomba apewe muda. Na huyu Bwana wake anaonesha msamaha kwa kumsamehe deni lote ambalo lilikuwa kubwa kuliko jinsi alivyo omba.

Lakini inaonekana alikuwa muigizaji mzuri sana kwasababu mara tu ya kusamehewa deni hili kubwa, anamkimbilia mtu ambaye alikuwa anamdai tena kiasi kidogo tu, na badala ya kumuonesha huruma “anamrukia na kuanza kumpiga, akimdai, nilipe mali yangu”. Msamaha kama ni wa kweli, unapaswa uingie kila mahali katika kila kitu tufanyacho.

Je, waweza kuona kosa lako na kusema samahani kwa mwingine?
Wakati unapo samehewa, jambo hili linatoa fundisho ghani?
Je, waweza kutoa msamaha na huruma kama wewe ulivyo samehewa?


Kama huwezi kjibu “ndio” kwa maswali hayo, basi ujue mfano huu uliandikwa kwa ajili yako. Haya ni maswali magumu kukutana nayo lakini ni maswali muhimu kama tunataka kutua mizigo na kuwa huru. Tutafakari maswali hayo hapo juu na katika sala tutafiti matendo yetu. Mimi na wewe tuna deni kubwa ambalo hatuwezi kulilipa (dhambi zetu). Bwana wetu anatuita leo katika mahakama yake (Ekaristi). Kwa msaada wa Roho Mtakatifu, tujenge tena upya uhusiano wetu na kuwa vyombo vya Amani.

Sala: Bwana, ninakiri dhambi zangu. Lakini ninakiri kwa msaada wa mwanga wa neema na huruma yako. Ninapo ipokea huruma hii katika maisha yangu, ninaomba unifanye mwenye huruma kwa wengine. Nisaidie niweze kutoa msamaha kwa uhuru kamili bila kubaki na kitu. Yesu nakumini wewe. Amina.


Copyright ©2013-2023 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.

No comments:

Post a Comment