MASOMO YA MISA, MACHI 24, 2023
IJUMAA, JUMA LA 4 LA KWARESIMA
SOMO 1
Hek. 2:1, 12-22
Wasiomsadikia Mungu walisema hivi, huku
wakimfikiri yasiyo kweli, Zaidi ya hayo na tumwotee mtu wa haki, maana hatuna
haja naye, naye yu kinyume cha matendo yetu; atukaripia ya kama tumeiasi
torati, na kutushitaki ya kama tumekosa adabu. Asema ya kwamba anamjua Mungu,
na kujiita mtumishi wa Bwana. Ametuwia magombezi ya fikira zetu. Hata kumtazama
twaona ni kugumu; maan amaisha yake si sawasawa na masiha ya wengine, na
mwenendo wake ni wa kigeni. Tuanhesabiwa naye kuwa kama madini hafifu;
anajitenga na njia zetu kama na uchafu. Wenye haki asema kuwa mwisho wao ni
heri; hujivuna ya kwamba Mungu ndiye baba yake.
Haya na tuone kama maneno yake ni kweli; tufanye
kujaribu yatakayompata wakati wa mwisho wake; mradi mwenye haki akiwa ni mwana
wa Mungu, Yeye atamtegemeza na kumwokoa mikononi mwa adui zake. Na tumhakikishe
kwa jeuri na maumivu, ili tujifunze upole wake na kuithibitisha saburi yake
akidhulumiwa. Hata tumhukumu auawe mauti ya aibu, maana ataangaliwa sawasawa na
maneno yake.
Ndivyo walivyosemezana, wakakosea kabisa. Kwa
maana uovu wao uliwapofusha; hawakuzijua siri za Mungu; wala hawakuutarajia
mshahara wa utakatifu, wala kudhani ya kwamba iko thawabu kwao wenye roho
zisizo na hatia.
Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 34:16-20, 22 (K) 18
(K) Bwana yu karibu nao waliovunjika moyo.
Uso wa Bwan ani juu ya watenda mabaya,
Aliondoe kumbukumbu lao duniani.
Walilia, naye Bwan akasikia,
Akawaponya na taabu zao zoe. (K)
Bwana yu karibu nao waliovunjika moyo,
Na waliopondeka roho huwaokoa.
Mateso ya mwenye haki ni mengi,
Lakini Bwana humponya nayo yote. (K)
Huihifadhi mifupa yake yote,
Haukuvunjika hata mmoja.
Bwana huzikombo a nafsi za watumishi wake,
Wala hawatahukumiwa wote wamkimbiliao. (K)
SHANGILIO
Lk. 8:15
Heri wale walishikao neno la Mungu katika moyo
wao mwema na mnyofu, na wazaao matunda katika uvumilivu.
INJILI
Yn. 7:1-2, 25-30
Baada ya hayo Yesu alikuwa akitembea katika
Galilaya; maana hakutaka kutembea katika Uyahudi, kwa sababu Wayahudi walikuw
awakitafuta kumwua.
Na sikukuu ya Wayahudi, Sikukuu ya Vibanda,
ilikuwa karibu. Hata ndugu zake walipokwisha kukwea kuiendea sikukuu, ndipo
yeye naye laipokwea, si kwa wazi bali kana kwamba kwa siri.
Basi baadhi ya watu wa yerusalemu wakasema, Je!
Huyu siye wanayemtafuta ili wamwue? Na kumbe! Anena waziwazi, wala hawamwambii
neno! Yamkini hao wakuu tuna jua hakika ya kuwa huyu ndiye Kristo? Lakini huyu
twamjua atokako; bali Kristo atakapokuja hakuna ajuaye atokako.
Basi Yesu akapaza sauti yake hekaluni, akifundisha
na kusema, Mimi mnanijua, na huko nitokako mnakujua; wala sikuja kwa nafsi
yangu; ila yeye aliyenipeleka ni wa kweli, msiyemjua ninyi. Mimi namjua, kwa
kuwa nimetoka kwake, naye ndiye aliyenituma.
Basi wakatafuta kumkamata; lakini hakuna mtu
aliyeunyosha mkono wake ili kumshika, kwa sababu saa yake ilikuwa haijaja bado.
Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
Copyright © 1993 T.M.P. Book Department, Tabora - Tanzania: see MASOMO YA
MISA. Scripture readings from ‘Biblia Takatifu’are published and copyright ©
1975, 1993 by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania.© Bible Society of
Kenya, © Bible Society of Tanzania.These readings are a reproduction by Furaha
ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment