“KWARESIMA YA UKARIMU”
Tafakari ya Kwaresima
Ijumaa, Machi, 24, 2023
Juma la 4 la Kwaresima
Hek 2: 1, 12-22;
Zab 34: 17-21, 23;
Yn 7: 1-2, 10, 25-30.
KUWEKA MAJARIBUNI
Kitabu cha Hekima kina kadiriwa kuandikwa miaka mia kabla ya kuja Kristo.
Lakini cha kushangaza maelezo yake yanaonekana kuwa karibu sana katika
kumwelezea Yesu. Somo la leo linaongelea kuhusu mtu ambaye anamjua Mungu na
hata anajiita “Mtumishi wa Mungu” (Hek 2:3). Na kama Yesu, huyu mtu ana adui
ambao wanamfuatilia ili kumtega katika maneno yake na hata kutaka kumua.
(2:19-20).
Leo tunakumbushwa kwamba kutakuwa na upinzani daima juu ya Kristo na wale
wanao mfuata. Katika somo la Injili, tunasoma, juu ya kushindwa kwa jaribio la
kumkamata Yesu wakati wa sikukuu ya Tabernaklo kwasababu “saa yake bado” (Yn
7:30). Ni kweli, Yesu alisulubiwa na kufa, lakini kifo hakikuweza kumweka
chini. Mungu alimfufua! Ndivyo hivyo sisi Mungu hataruhusu kitu tunacho vumilia
kituangushe bila kutusaidia. Atatuimarisha. Atatupa neema. Atatuinua tena.
Yesu anatuita sisi tuwe mabalozi wake. Anatutaka sisi tushirikishe habari
njema kwa kila mtu tunae kutana naye. Huu ndio wito wa pekee, lakini pia kuna
changamoto zake. Pengine juhudi zetu zitafanikiwa baada ya kupata upinzani
mkubwa na majaribu makubwa, na hata changamoto nyingine ni za kusukumwa. Lakini
tukibaki imara katika kushirikisha Injili kwa upendo na sio kwa kujiona wema
wenyewe, kwa furaha na sio hasira, tutabarikiwa sana. Yesu atatuambia “vyema
mtumwa mwema ingia katika furaha ya Bwana wako” (Mt 25:21). Hauhitaji kuwa mtu
uliye bobea katika kuongea au kuwa mashuhuri katika kuongea. Wala haupaswi kuwa
na nguvu labda nyingine. Tunapaswa kutambua tu Yesu anatupa nguvu na neema
tunapo amua kumshuhudia. Na neema yake itatutunza kama ilivyo na nguvu ya
kuwavuta watu kwake.
Sala: Bwana, nakupenda. Nisaidie nikuone na kukupenda wewe katika jirani
zangu. Nisaidie ninapo wekwa katika majaribu, na familia yangu, marafiki zangu,
na wengine wanao nipinga kwasababu ya kukutangaza wewe na thamani ya Injili
yako. Tufariji daima tunapo tangaza Injili yako. Tupe nguvu yako ya Kimungu.
Yesu nakuamini wewe. Amina
No comments:
Post a Comment