“KWARESIMA YA UKARIMU”
Tafakari ya Kwaresima
Jumapili, Machi 5, 2023.
Dominika ya 2 ya Kwaresima
Mwa 1:1-4;
Zab 33:4-5, 18-22;
2 Tim 1:8-10;
Mt 17: 1-9.
KWARESIMA: MUDA WA KUMFAHAMU YESU!
Juma la kwanza la Kwaresima linatuandaa, kufanya matendo ya kwaresima,
kusali, kufunga na kutoa sadaka. Inakuwa ni hatua kwetu kutengeneza hali nzuri
ya kuingia katika kipindi hichi kwa undani. Jumapili iliopita ilituandaa kuhusu
majaribu, na umuhimu wa kusafisha dhambi zetu rohoni mwetu. Yesu alituanyesha
njia ya kumshinda shetani na dunia na pia vishawishi vya miili yetu, alipokuwa
jangwani. Leo anajifunua kwa njia ya Kugeuka sura kutualika wote kwenye utukufu
alio nao na Baba yake. Kwa njia ya kungara sura tunaalikwa kwenye ufufuko wa
miili, wakati tutakapo kuwa huru kuhusu dhambi. Kama mwili wa Yesu ulivyokuwa
katika utukufu, ndivyo miili ya watakatifu itangaa. “Utukufu ulionipa mimi
nimewapa wao” (Yn 17:22).
Uhusiano unakuwa kadiri ya muda. Tunawafahamu watu zaidi kadiri ya muda
unavyo sogea. Mitume pia lazima na wao waliendelea kumfahamu Yesu kadiri ya muda
ulivyokuwa ukisogea. Uhusiano wao ulianza alivyo waita hapo awali. Waliishi
naye na kumsikiliza na kushuhudia miujiza na uponyaji mbali mbali. Uelewa wao
lazima utakuwa ulikuwa kadiri ya muda, mpaka Petro akafikia kiwango cha kusema
“Wewe ni Masiha Mwana wa Mungu aliye hai”. Lakini Petro alimpinga alivyosikia
habari ya kifo chake, na Yesu alitambua kuwa Wafuasi wake hawajamfahamu vizuri
bado. Walimwelewa vibaya kuwa kama Masiha wa kidunia atakaye iongoza dunia
daima. Ndio, maana baada ya siku sita hivi Yesu awaliwachagua Petro, Yohane na
Yakobo kwenda mlima na kushuhudia kungara kwake kwa sura inayoelezewa leo
katika Injili.
Kungara sura kwa Yesu kunatokea wakiwa juu ya milima. Mlimani palijulikna
kama sehemu ya kukutana na Mungu. Wakati Yesu anageuka sura mavazi yake
yalingaa sana na uso wake ulingara. Taswira hii alioionyesha Yesu ni hali ya
utukufu ambayo itakuja baada ya maisha ya ulimwengu huu. Musa na Elia ambao
katika tamaduni ya Wayahudi waliwakilisha mambo mawili muhimu ya Wayahudi.
Sheria na Manabii. Musa na Elia walikuwa ni watu ambao walipata kuwasiliana na
Mungu wakiwa katika milima. Na waliwaongoza watu wa Israeli kumrudia Mungu.
Kwa kuangalia hali hii ya kugusa na kuogopesha, Petro anaomba kujengwe
vibanda vitatu kimoja cha Yesu, kimoja cha Elia na kimoja cha Musa. Petro
alipenda hii hali iendelee kuwapo. Mungu anaingia kati na kumfunua mwanae
(Mwana wa Mungu) kwa wafuasi “Huyu ndiye Mwanangu mpendwa…” Mitume wanaogopa na
wanainamisha nyuso zao. Walivyo nyanyuka walikuta kila kitu kikiwa katika hali
yakawaida. Tukio hili ni lazima lilikuwa ni la nguvu sana kuliko tukio lolote
lile ambalo mitume hawa watatu waliweza kulishuhudia. Katika tukio hili la
kungara sura, Umungu wa Yesu ulifunuliwa kwao. Waliweza kufahamu Yesu ni nani
na kwanini Yesu alikuwa akiongelea kuhusu kifo na ufufuko . wafuasi waliweza
kuja kumfahamu Yesu vizuri zaidi wakati wa Karamu ya mwisho, mateso yake
alivyokuwa pale Getsemane, mateso yake, kifo na kufufuka. Muda wote waliokuwa
na Yesu waliweza kuja kumfahamu Yesu na kutambua nini maana ya kuwa wafuasi.
Nasi ni hivyo hivyo.
Katika somo la kwanza tunasikia kuhusu kuitwa kwa Abrahamu. Abrahamu
anajibu wito wa kwanza kabisa wa Mungu. Na ni baada ya muda tu alikuja
kumfahamu Mungu vizuri na utume wake kwa ajili yake. Hivyo, tunavyopata muda wa
kuwa na Mungu zaidi ndivyo tunavyozidi kuendelea kumfahamu zaidi, na kadiri
tunayo endelea kumfahamu Mungu, ndivyo tunavyo fahamu mpango wake kwetu.
Kwaresima ni kipindi cha kutafakari na kukaribisha neema ya Mungu katika
maisha yetu. Sio muda tu wakuachia vitu, bali pia ni muda wakupokea zawadi
kubwa kutoka kwa Mungu. Mungu hajatusahau sisi watoto wake ila ni sisi
tuliomsahau yeye na kukimbia uso wake. Leo, upendo unafunuliwa kwetu kwa njia
ya Yesu. Yesu kwa njia ya ufufuko anatufanya sisi kuwa sehemu ya mpango wa
Mungu tangu milele, kuwa watakatifu na kupendwa na Mungu kwa kuwa daima mbele
zake. Ufufuko unaleta kwetu mwanga katika maisha yetu kama wa kungara sura kwa
Yesu, kiasi kwamba hakuna giza linalo baki.
Maandiko matakatifu yanatuonesha njia ya kwenda katika muelekeo huu. Kwanza
kabisa, kuwa na muda wa kusali kama Yesu. Pili ni kumfahamu Yesu, na hili
linafanyika kwa kutafakari Maandiko Matakatifu, Mungu aliwaambia wafuasi kwamba
“Msikilizeni yeye” pia Neno la Mungu linafunua nafsi ya Yesu kwetu sisi kila
siku. Tatu, tuwe tumeungana katika jumuiya zetu. Kama mitume watatu walivyo
pata kumshuhudia Yesu, na kushiriki katika mwanga uliofunuliwa na Mungu. Hili
linawezekana daima tunavyo shiriki katika Ekaristi Takatifu, tunaitwa wote
kuunganika katika kungara kwa Yesu katika Ekaristi takatifu. Na mwisho kabisa,
kushiriki katika mahusiano mazuri na wenzetu. Mitume hawakuweza kushirikisha
walio yaona muda ule, bali walishirikisha baada ya ufufuko wakati wamesha elewa
maana kamili ya kungara kwake sura, walishirikisha wengine kwa kuhubiri habari
Njema. Sisi pia tunaitwa kutangaza kungara kwa sura kwa Yesu kwa kuwatangazia
wale wote waliotengwa. Tunaitwa kutambua matendo ya roho na matendo ya nje ya
huruma: kuwalisha maskini, kuwapa maji walio na kiu, kuwavisha wasio na nguo,
kuwakaribisha wasio na makao, kuwaponya wagonjwa, kutembelea wafungwa, kuwazika
wafu, , kuwasaidia walio na mashaka, kuwaelekeza walio wajinga, kuwa elekeza
wadhambi warudi, kuwafariji wenye matatizo, kuwasamehe walio tukosea,
kuchukuliana kwa huruma wale wote wanao tuumiza na kuwaombea walio wazima na
wafu.
Sala: Bwana, ninaomba nifarijike kwa utukufu wako na ukweli wako. Ninaomba
nikumbuke utukufu huu ninapo tembea katika changamoto mbali mbali katika
maisha. Utatembea mbele yangu na kunitangulia nikikuamini wewe. Yesu, nakuamini
wewe. Amina.
No comments:
Post a Comment