“KWARESIMA YA UKARIMU”
Tafakari ya Kwaresima
Jumamosi, Februari 21, 2026
Jumamosi baada ya Jumatano ya majivu
Isa 58: 9-14;
Zab 86: 1-6;
Lk 5: 27-32
KUMTEMBELEA DAKTARI YA MIOYO YETU!
Roho ya kweli ya Kwaresima ni, kufunga, kutoa sadaka na sala, yote haya
yamejengwa juu ya kwenda kinyume na matamanio yetu, na kutamani kuwa na Mungu
katika Ufalme wake. Hii haina maana kwamba mmoja anapaswa kuacha kwa muda wa
siku 40 ili awasaidie maskini wakati wa Kwaresima tu. Tunapaswa kuelewa nafasi
mbali mbali zinazokuja katika maisha yetu ya kila siku. Ni muda pia wa kuacha
dhambi na kupokea uponyaji kutoka kwa mganga mtakatifu.
Yesu aliwahitaji wadhambi. Yeye ni mkombozi, na mkombozi aliwahitaji wadhambi
ili awakomboe! Kuja kwa Yesu tukiwa na mizigo ya dhambi zetu, inampa furaha
katika moyo wake. Anafurahi kwasababu anatimiza ule utume aliotumwa na Baba
yake, akionesha kuruma yake kama Mkombozi pekee. Muacha akupe huruma yake!
Unafanya hivi kwa kuja kwake katika hali yako ya dhambi na kujinyenyekesha
mbele kama asiestahili huruma yake, na ambaye unastahili tu hukumu. Kuja kwa
Yesu inamfanya yeye aweze kuonesha huruma yake kutoka katika chemchemi ya
huruma yake.
Angalia katika hali ya kwamba Yesu ni Mganga Mtakatifu anayekusubiri ili
aweze kutimiza wajibu wake wa kuponya. Anakuhitaji wewe ukubali dhambi zako na
kuwa wazi kwa uponyaji wake. Kwa kufanya hivyo, unaruhusu mlango wa huruma yake
ufunguke na kumimina baraka kwako na katika kipindi chetu.
Sala: Mpendwa Mkombozi na Mganga Mtakatifu, ninakushukuru kwa kuja
kutukomboa na kutuponya. Ninakushukuru kwa tamaa yako ya kuonesha huruma yako
katika maisha yangu. Naomba uninyenyekeshe niweze kuwa wazi kwa uponyaji wako.
Yesu nakuamini wewe. Amina

No comments:
Post a Comment