Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

JUMA LA NNE LA KWARESMA - NJIA YA MSALABA



Njia ya msalaba inaashiria njia ya mateso ambayo Yesu aliifanya pamoja na msalaba kufa Kalvari. Kanisa linafundisha kuwa Roho Toharani zinapitia hali za utakaso ambazo lazima ziambatane na mateso. Kwa kusali na kutoa sadaka kwa ajili ya Roho Takatifu, unakuwa na nguvu kubwa na fulsa ya kuondoa maumivu yao. Katika kurejesha, shukrani zao zitakuletea Baraka nyingi. Basi bubujiko la huruma libubujike kutoka kwako kwenda kwa Roho Takatifu Toharani.


TENDO LA KUOMBA MSAMAHA

Yesu wangu, nakupenda wewe zaidi ya vitu vyote. Ninazichukia na kutozipenda dhambi zangu zote, kwasababu ya hizo nimekukosea wewe. Furaha takatifu, matunda na hasara za uchaji huu ninakusudia kuupata kwaajili ya roho Toharani, hususani kwaajili ya wote waliopo motoni waliokuwa karibu na wapendwa wangu, na pia kwa wale wote ambao nipo kwaajili yao, kwa namna ya pekee, napaswa kusali. Ee Maria, mama yangu wa huruma na mama wa roho masikini zilizopo toharani nisindikize mimi, kwa maombezi yako katika safari hii.


Kabla ya kila kituo:
K: Ee Yesu tunakuabudu, tunakushukuru;
W: Kwa kuwa umewakomboa watu kwa msalaba wako mtakatifu.

Baada ya kila kituo:
'Baba Yetu, 'Salamu Maria' na 'Atukuzwe Baba',
K: Ee Bwana utuhurumie! W: Utuhurumie!

K: Roho za waamini marehemu, wapate rehema kwa Mungu, wapumzike kwa amani. W: Amina


1. KITUO CHA KWANZA - YESU ANAHUKUMIWA AFE

Ee Yesu wangu usiye na hatia, kuniweka huru kutoka katika kifo cha milele, ulijiruhusu mwenyewe kulaumiwa na hukumu ya toharani mpaka kifo msalabani. Nijalie kuchukia dhambi na neema za kuishi ili siku moja niipate toka kwako hukumu ya huruma. Roho masikini Toharani zimeshahukumiwa. Kupitia huruma yako wameikwepa jehanamu, lakini katika hesabu ya dhambi zao haki yako iliwapeleka katika moto wa Toharani. Ee Yesu mkuu wa huruma wahurumie.  Ondoa hukumu yao ya kuwatenganisha na wafungulie milango ya mbinguni.


2. KITUO CHA PILI - YESU ANAPOKEA MSALABA
Ee msalaba mtakatifu, ndio mti wa uhai, lango la mbinguni, ukombozi wetu na tumaini letu pekee.
Kuwa mkombozi wangu katika saa ya kufa. Ee Yesu, waangalie watumishi wako waliofariki toka maisha haya kwa ishara hii ya imani. Wape uhuru kwa nguvu ya ushindi wa msalaba wako, ambapo kwa njia yake ulishinda mauti.  Waongoze katika maisha na furaha ya milele.


3. KITUO CHA TATU - YESU ANAANGUKA MARA YA KWANZA

Kupitia udhaifu wako chini ya msalaba na faida za kuanguka huku kwa kwanza, nisaidie mimi uvumilivu katika maamuzi yangu mapya ili daima niweze kutembea kwa uaminifu katika njia zako takatifu. Roho Toharani sasa zinateseka kwasababu zilipuuzia na kutumia vibaya neema zako katika maisha haya. Sasa zinatambua kuwa hakuna roho yenye dhambi inayoweza kumuona Mungu. Hivyo kuwa na huruma juu yao, hivyo na zitakase kutoka katika dhambi zote. Kupitia maombezi ya Mama yako wa huruma, waokoe kutoka Toharani. 


4. KITUO CHA NNE - YESU ANAKUTANA NA MAMA YAKA

Ee Moyo wa Maria! Ee  moyo wa Yesu! Nayatoa maisha yangu kwa ajili ya dhambi zangu. Majina mazuri ya Yesu na Maria yawe katika mdomo wangu na ndani ya moyo wangu katika saa ya kifo. “Ee moyo mwema wa Yesu, tunaomba ili tuweze kukupenda wewe zaidi na zaidi.” Moyo mwema wa Maria kuwa ukombozi wetu.” Mama mwenye huruma sana, bikira wa huruma wa Roho Takatifu, mikononi mwako naziweka sifa zangu na kukuomba uziunganishe na sifa zisizoisha za Mwanao. Zitoe daima katika mikono ya Mungu kwaajili ya roho zote zinazofungwa kwangu kwa vifungo vya mahusiano.


5. KITUO CHA TANO - SIMONI WA KIRENE ANABEBESHWA MSALABA AUCHUKUE NYUMA YA YESU

Ee Yesu wangu, ninaukubali msalaba, ninaukumbatia. Niwezeshe nikusaidie kuubeba msalaba wako, kwa kuwa mvumilivu katika majaribu yote ambayo yanaweza kunivamia mimi. Ni roho ngapi sasa Toharani zinajutia hali zao za zamani za kutokuwa na uvumilivu! Lakini wewe, Ee Bwana, kuwa mkarimu kwao zilipe zote zinazoendelea kuomba msamaha.


6. KITUO CHA SITA - VERONIKA ANAUPANGUSA USO WA YESU

Bwana, Yesu Kristo, wewe uliyeacha alama ya damu yako ya uvumilivu juu ya kitambaa cha Veronica, saidia ili kumbukumbu ya mateso yako machungu na kifo viweze kubakia na kuridhisha nafsi yangu. Zihurumie roho masikini, zifanye katika taswira yako na ufanano wako na kuokolewa kwa Damu yako Takatifu. Ziweke huru kutoka katika dhambi zote ili ziweze kuingia mbinguni na kukuona wewe ana kwa ana daima na milele.


7. KITUO CHA SABA - YESU ANAANGUKA MARA YA PILI
Ee Yesu, dhambi zangu zimeufanya msalaba wako kuwa mzito. SIzipendi na hakika ninaamua kuyarekebisha maisha yangu. Usiniruhusu kamwe kutengana nawe tena. Ee Yesu nihurumie, kwa ajili ya nafsi zote zitesekazo maumivu ya Toharani kwa ajili ya dhambi ya mauti walizozifanya katika maisha haya. Ee moyo mwema wa Yesu, kuwa na huruma juu yao.


8. KITUO CHA NANE - AKINA MAMA WANAMLILIA YESU

Moyo wa Yesu uliojawa na huruma! Yesu wangu, uliyesema kwa mama mtakatifu: “Msinililie mimi, bali lieni kwaajili yenu na kwa ajili ya watoto wenu,” nifanye nilie kwa ajili ya wasio na shukrani, ambayo nimeirudisha kwaajili ya upendo wako. Nategemea kufidia maisha aya kwa ajili ya dhambi zangu, ili nipate msamaha wao baada ya hapo. Nikirimie upendo wa ukarimu kwaajili ya nafsi zilizopo Toharani, hususani kwa ajili ya dhambi za ndugu zangu. Ninaahidi kwa ajili ya siku za baadae kutenda kile nilichokiacha kupitia usahaulifu wangu na ugumu wa moyo.


9.  KITUO CHA TISA - YESU ANAANGUKA MARA YA TATU

Kupitia kuanguka huku kwenye maumivu sana, Ee Yesu, ninakuomba uniokoe kutoka katika kifo kisicho cha furaha, ambacho kinaweza kunipeleka jehanamu. Kutoka katika nguvu za adui, iokoe roho yangu ya umauti, na nifanye niishi na nife katika neema zako. Ziangalie kwa huruma roho zote masikini zijitesazo ndani ya Toharani. Kwa machozi na sala zinaomba msaada wako na huruma yako. Zisikilize sala zao na waongoze nje sehemu ya mateso kwenda sehemu ya mbinguni iliyobarikiwa, huko kufurahia daima utukufu wa makuu yako.


10. KITUO CHA KUMI - YESU ANAVULIWA NGUO

Mkombozi wangu mbarikiwa, ulivuliwa nguo kwaajili ya upendo kwangu, nijarie unyenyekevu na usafi mtakatifu. Niokoe kutoka katika tabia zote za kuunda vitu: nifanye nife katika kila kitu cha ulimwengu huu, ila katika utengano wa kifo kutoka katika vitu vyote vya ulimwengu uwe rahisi. Katika faida gani sasa mali na starehe za dunia hii kwenye roho za Toharani? Miili yao walipaswa waiache katika raha, na mali zao kwa warithi; ni kazi zao pekee zimewafuata, wema wazawadiwe, ovu liadhibiwe. Ee Bwana, fikisha kikomo mateso yao, wala usiwawekee urefu katika warithi wa watakatifu, lakini wasamehe na wasajiri katika ufalme wa milele wa mbinguni na furaha.


11. KITUO CHA KUMI NA MOJA - YESU ANASULUBISHWA MSALABANI

Yesu wangu usiye na hatia, ulisurubiwa msalabani kwaajili ya dhambi zangu, ninakuomba wewe, kupitia sifa za mateso yako matakatifu, uje katika msaada wangu katika kuumwa na mateso yangu ya mwisho. Nijarie neema nizipokee kwa muda Sakramenti zako kuu. Njoo kwangu Ekaristi Takatifu, na nimiminie moyoni mwangu uvumilivu wa Moyo wako Mtakatifu! Na wewe, Ee Maria Mama, nifariji katika saa hili na yafanye matamu mateso yangu, kupitia huzuni iliyoikandamiza moyo wako wakati wa kusuribiwa. Mwana kondoo wa Mungu, zihurumie roho zote Toharani, ambazo mateso yake ni makubwa zaidi ya wote wagonjwa na wanaokufa. Wanusuru katika mateso haya, na kupitia thamani ya mateso yako wapokee katika makao ya milele.


12. KITUO CHA KUMI NA MBILI - YESU ANAKUFA MSALABANI

Kupitia masaa matatu ya mateso msalabani, nikirimie mimi, Ee Yesu, kifo cha furaha. Nichukue pale nitakapokuwa nimejiandaa vizuri. Katika saa hiyo ijaze roho yangu kwa hisia takatifu za kiimani, tumaini na upendo. Nijarie kuomba msamaha wa kweli kwaajili ya dhambi zangu na neema kukubali pamoja na kukubali Kikristo kifo changu pamoja na maumivu na mateso yake yote. Nifanye niuache ulimwengu huu nikilitamka Jina lako Takatifu. Maria Mama wa Huruma, kimbilio la wanaokufa, kuwa karibu nami katika mateso yangu ya mwisho. Kumbuka, Ee Yesu mwenye upendo, roho masikini zenye upendo huo ambazo kwa huo ulitoa faraja kwa mwizi mwema: “Leo utakuwa nami Peponi.” Ziite roho hizi katika ufalme wa utukufu wako, ili ziweze kukusifu wewe pamoja na malaika na watakatifu wote daima na milele.


13. KITUO CHA KUMI NA TATU - YESU ANASHUSHWA MSALABANI

Yesu, wewe ambaye roho yako ilishuka kwa wafu kuitangaza amani kwa watu wenye haki kwa Agano la Kale, shuka sasa kati ya roho masikini zikutafutazo wewe; waweke huru katika minyororo ya utumwa wao na wakirimie uhuru wa watoto wakweli wa Mungu! Ee Maria, Mama yangu, niwezeshe kama Yesu, niwekwe katika mikono yako wakati wangu wa kuondoka kutoka katika ulimwengu huu. Kuwa nami wakati wa Hukumu Takatifu ili kupitia maombezi yako, niweze kupata hukumu njema yenye huruma. Moyo Mtakatifu wa Maria kuwa mkombozi wangu!


14. KITUO CHA KUMI NA NNE - YESU ANAZIKWA KABURINI

Yesu, kupitia fadhila za mateso na kifo chako chenye uchungu na kupitia Ufufuko wako mtukufu, ninakuomba wewe, kuwa na huruma kwa roho zote masikini na zijarie furaha na usajiri wa utukufu huko mbinguni. Wawezeshe waingie katika amani hiyo waliyoitamani kwa muda mrefu; wafanye watafakari utukufu wa Maono Matakatifu; basi ruhusu wabariki huruma yako milele. “Moyo wa Maria, kuwa mkombozi wangu,” pale mimi mwenyewe nitakapofika katika sehemu ya mateso, wakati mwili wangu utakapokuwa katika dunia baridi na roho yangu katika moto wa Toharani. Mama wa upendo, okoa watoto wako katika siku hiyo. Nikirimie unafuu wa mapema na kupitia thamani zako niokoe kutoka katika moto, ili niweze kukushukuru mbinguni, pamoja na wewe na watakatifu wote, abudu na mpende Yesu, Mwanao mpendwa, ambaye pamoja na Baba na Roho Mtakatifu waishi na kutawala, Mungu wa kweli, daima na milele. Amina.


SALA YA MWISHO

Mkombozi wangu msuribiwa, ninakutolea kazi hii ya uchaji, ambayo kwa neema yako, nimeimaliza hivi punde. Jaria matunda mazuri ya kifo chako juu msalabani yasipotee kwaajili yangu au kwaajili ya roho Toharani. Maria, Mama wa Huruma, yaweke maombi yangu katika Moyo wa Mwanao mpendwa wako, ili niweze kusajiliwa katika ufalme wa neema, huko pamoja na wapendwa wangu, wote waishio na wafu, tuweze kubarikiwa daima.

Moyo mkunjufu wa Yesu, uliyepo daima katika Sakramenti Takatifu, iangazayo kwa upendo uwakao kwa roho masikini zilizofungwa Toharani, zihurumie. Usiwe mkali katika hukumu zako, lakini zifanye baadhi ya matone ya Damu yako Takatifu yaanguke katika moto uangamizao, na Ee Mkombozi wa Huruma, tuma malaika wako waongoze katika nafasi ya hamasa, mwanga na amani. Amina.


KWA AJILI YA NIA ZA BABA MTAKATIFU
'Baba Yetu, 'Salamu Maria' na 'Atukuzwe Baba',


K: Roho za waamini marehemu, wapate rehema kwa Mungu, wapumzike kwa amani. W: Amina

No comments:

Post a Comment