“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Jumamosi, Februari 4, 2023
Juma la 4 la Mwaka wa Kanisa
Ebr 13: 15-17, 20-21;
Zab 22: 1-6;
Mk 6: 30-34.
YESU MWENYE HURUMA!
Yesu ni kiongozi bora mwenye huruma kwa wanyonge katika jamii, mwenye
huruma pia kuelekea mahitaji ya binadamu. Baada ya Wanafunzi kurudi kutoka
utume kuhubiri, Yesu anapendekeza wapumzike. Lakini yeye mwenyewe, akiacha
mahitaji yake kama kupumzika, chakula, nk, alianza kuwahudumia watu, kwa sababu
walikuwa na uhitaji mkubwa zaidi. Binadamu kwa kawaida tena mara nying
anajifikiria yeye kwanza,( binafsi); na anatimiza mahitaji yake kwanza. Lakini
Yesu ni mfano halisi wa kutokuwa na ubinafsi.
Jibu la Yesu linaonesha moyo wenye huruma. Anasukumwa na huruma kwa ajili
yao na anaendelea kuwafundisha mambo mengi. Haya yanatokea kwasababu ya sababu
nyingi. Kwanza, kwa sababu ya hamu kubwa ya ndani ya watu kuhusu yeye.
Walivutwa kwa Yesu, kumsikiliza na kujifunza kwake. Pili, ni kwasababu Yesu
alikuwa na hamu kubwa ya kuwa na watu wake. Alitamani kushirikisha moyo wake na
wao na kuwachunga kama mchungaji, kuwaongoza kwenye ukweli aliokuja kuufunua.
Yesu alikuwa Mchungaji wa kweli aliye wapenda kondoo wake na kuwakaribisha
daima.
Inapaswa iwe hivi pia kwetu sisi. Tunapaswa tutafute daima kuwa naye,
kumpenda na kufuata amri zake. Tunapaswa kujitoa bila kuchoka kumtafuta bila
kujali ni ugumu ghani tuna upata. Tuna jukumu, kwa upendo tumtafute na kumpata
Bwana wetu. Na Yesu, atafanya jukumu lake la kutuchunga na kutuongoza kama
mchungaji na kutufundisha mambo mengi. Ataruhusu moyo wake uongozwe na huruma
juu yetu na kutuvuta karibu naye.
Kuna msichana mmoja, alikuwa anarudi kutoka shuleni, kwa miguu akiwa pamoja
na wadogo zake wawili wakiume. Ghafla theluji ikaanguka ya kutisha. Wakaona
kifo kipo mbele yao. Yule Msichana akatoa zile nguo zake mwenyewe za kuzuia
baridi akawafunika kaka zake ndani ya nguo zile akawakumbatia, kuwalinda, kama
vile alivyoweza, na mwili wake mwenyewe. Badaaye, wazazi wakatoka kwenda
kuwatafuta watoto,wakawakuta wale wavulana hai na dada yao amekufa. Wenyeji wa
kijiji kile wakajenga mnara wa kumbukumbu pale, wakaandika "Msukumo
kwaajili ya kulinda uhai". Je! Imani yako kwa Yesu inakuongoza ufanye nini
? Leo Yesu anatukaribisha na kutuongoza tumuige yeye, je upo tayari?
Sala: Bwana, nakupenda wewe na ninatoa maisha yangu kwako. Ninakuomba
unijaze daima na na moto wa kutaka kukutafuta kila siku. Ninakushukuru kwa
huruma yako na uchungaji wa roho yangu. Ninaomba nijipumzishe karibu na moyo
wako daima. Yesu nakuamini wewe. Amina
No comments:
Post a Comment