“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Jumatatu, Februari 20, 2023
Juma la 7 la mwaka wa Kanisa
YbS 1: 1-10;
Zab 93: 1-2, 5;
Mk 9: 14-29.
NGUVU YA AJABU YA IMANI!
Swala wa Kiafrika anauwezo wa kuruka juu uwezo wa 10ft, ingawaje anaonekana
ni kiumbe mdogo, mwenye urefu wa 3-4ft, katika mbuga za wanyama au zuu,
wanajenga ukuta wa urefu wa 4ft kwenda juu. Kwanini? Ni kwasababu swala hawezi
kuruka kizingiti bila kufahamu na kuona miguu yake itatua wapi baada ya kuruka.
Ni kweli pia ukilinganisha na imani yetu kwa Mungu. Tunakuwa na imani tu pale
tunapo elewa kitu.
Kuna sentensi yenye kushangaza kutoka katika Injili ya leo anayo ongea mtu
mmoja. Alimwambia Yesu “nina imani. Nisaidie kwa imani kidogo nilio nayo!”.
Kwamba huyu mtu alimfahamu Yesu kabla au la ni vigumu kusema. Bali aliweza
kutoa ufupisho wa kitu ambacho ni kipingamizi kikubwa kwetu Wakristo katika
kukuwa katika maisha ya Kiroho, ambayo ni imani yenye mashaka, imani isio
kamilika. Huyu mtu alisema ukweli na undani wake kwamba, ingawaje ana amini
ambacho Yesu anaweza kusema na kufanya, lakini bado amejazwa na mashaka.
Alikuwa akianguka kwenye imani yake yenye wasi wasi. Na kwasababu alikuwa
akikabiliana na ukosefu wake wa imani, alipata baraka nyingi. Sentensi
iliosemwa na mtu huyu ilikuwa sentensi ya uaminifu. Ilikuwa ni sentensi ya
kujali na pia ukweli wa imani yake.
Kama tunataka kukuwa katika Kristo, ni vizuri kutambua na kukiri kwamba
huenda hatumuamini Yesu vizuri kama inavyo paswa au kama tunavyopenda iwe. Kitu
kizuri na cha kweli ni kusimama mbele ya Yesu na kukiri kutoka ndani kabisa mwa
mioyo yetu kwamba “ninakuamini Bwana, ila nakuomba unisaidie na kutokuamini
kwangu”.
Sala: Bwana, ninaomba nije kwako katika hali zote. Ninaomba nikupende na
kukutumikia wakati maisha yakiwa mazuri, wakati maisha yana mawimbi na misuko
suko na changamoto. Niongezee imani na unisaidie niweze kuidhihirisha imani
hiyo katika maisha yangu. Yesu, nakuamini wewe. Amina.
No comments:
Post a Comment